Showing posts with label Kitaifa. Show all posts
Showing posts with label Kitaifa. Show all posts

Sunday, June 22, 2014

Kutoka Mjengoni : Sitta awahakikishia Watanzania kupata katiba ya kuwalinda wannyonge


Dodoma. Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amechaguliwa kwa kishindo kuliongoza Bunge Maalumu la Katiba, huku akisema kuchaguliwa kwake ni sawa na kumrudisha chura kwenye dimbwi la maji.
Jana, Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), alipata kura 487 na kumbwaga mpinzani wake, Hashimu Rungwe wa Chama cha Ukombozi wa Umma aliyepata kura 69.