TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inaendelea kufanya vibaya katika michuano mbalimbali, ikiwemo ya mashindano na ile ya kirafiki ambayo kimsingi ndiyo nguzo muhimu kwa timu hiyo kukua na kuendelea.
Nimekuwa mmoja wa watu waliokuwa karibu na Taifa Stars kwa misingi kwamba naifuatilia katika michuano yake mbalimbali, iwe ya nje au ile inayochezwa kwenye ardhi ya Tanzania.
Ninachokiona kwangu ni kitu kimoja kwamba kikosi cha Stars kina matatizo mengi, hasa ya uteuzi wa timu yenyewe ambayo kimsingi kimekuwa kiini cha matatizo ya timu hii ambayo ndiyo roho na kioo cha nchi katika sura ya kimataifa.
Tangi enzi za Kocha wa zamani wa timu hiyo, Marcio Maximo, kikosi hiki kimekuwa kina matatizo ya uteuzi na Watanzania wamekuwa wakijiuliza ni sifa gani ambazo zilikuwa zikitumika katika kuteua kikosi hicho.
Miongoni mwa wachezaji ambao watu walijiuliza kwa nini hawaitwi wakati walikuwa na uwezo ni kipa Juma Kaseja, ambaye alicheza muda mfupi sana akiwa na kikosi cha Stars, lakini mbadala wake alikuwa ni Ivo Mapunda.
Hata hivyo, ilipotokea Mapunda hayupo, aliyekuwa anapewa jukumu la kukaa langoni alikuwa ni Ally Mustafa ‘Barthez’, ingawa kwa wakati huo hakuwa akipata nafasi kwenye kikosi cha Simba alichokuwa akikitumikia.
Lakini baada ya kumalizika kwa utawala wa Maximo kwa muda wa miaka minne bila kombe lolote, aliyekuja kuchukua nafasi yake, Jan Poulsen, aliwaita wachezaji wote kadri ilivyowezekana, hali ambayo iliweza kumsaidia kupata ubingwa wa Chalenji mwaka 2010.
Lakini baada ya hapo hatukuweza kushiriki fainali zozote kubwa, lakini wengi wa Watanzania pamoja na mimi niliamini kuwa kuna uwezekano wa kupatikana kwa matumaini kwa siku zijazo kama nchi, kwa maana kupata nafasi ya kushiriki japo michuano ya Afrika, yaani Afcon au ile ya wachezaji wa ndani, maarufu kama Chan, pia hilo tulilishindwa.
Ila kwa sababu wakati wa Babu Poulsen kulikuwa na mipango mizuri ya kuendeleza soka la vijana ambapo kulikuwa na msaidizi wake ambaye alikuja kuwa kocha mkuu, Kim Poulsen, wakati wa muunganiko huu tuliona mabadiliko makubwa kwenye timu ya taifa, ambapo zaidi walikuwa wakitumika vijana na timu ilikuwa na damu mchanganyiko.
Hii ilikuwa ni hatua moja mbele, lakini baada ya kuondoka kwa Jan pamoja na Kim, tunaanza kurudi kule kule kwamba timu ikaanza kupoteza hamasa kwa mashabiki na kuitwa kwa kikosi kukawa na ukakasi ambao hadi sasa umeendelea kuwepo, jambo ambalo kimsingi linafanya kurudi nyuma badala ya kwenda mbele kama zilivyo nchi nyingine.
Kwa mfano, katika kikosi cha mwaka huu ambacho kimekwenda kwenye michuano ya nchi za Kusini mwa Afrika, yaani Cosafa, kimelalamikiwa na kuwa na lawama nyingi kwa dawati la ufundi lililopo chini ya Kocha Mart Nooij, kwa kuachwa kwa baadhi ya wachezaji wenye uwezo na kuitwa wale ambao kimsingi hata katika ligi hawachezi au hawapo katika kikosi cha kwanza.
Kwa mfano, mchezaji kiungo kama Amri Kiemba ambaye kwenye kikosi cha Azam FC hana namba kwenye kikosi cha kwanza, lakini ameitwa huku ligi amekuwa hachezi mara kwa mara. Hali hii ipo sawa na John Bocco, ambaye pamoja na kuwa nahodha, lakini hayupo kwenye kikosi cha kwanza cha Azam FC.
Kwa upande wa makipa, Mwadini Ally na Deo Munishi ‘Dida’ wanaitwa, lakini wapo wachezaji waliofanya vizuri zaidi ikilinganishwa na wachezaji hao tena kwa kucheza mechi nyingi.
Kwa mfano Barthez anaacha kuitwa wakati yeye ndiye kipa namba moja kwenye kikosi cha Yanga, hapa ndipo ninapoona tatizo la Stars ni kubwa kuliko linavyotazamwa, kwani inawezekana kabisa Nooij, wasaidizi wake hawamsaidii kama inavyotakiwa, ndiyo maana amekuwa akiita wachezaji wasiostahili na kuacha wale wenye sifa.
Iinakuwaje leo hii unamuita Bocco mwenye mabao matatu kwenye ligi, lakini Rashid Mandawa mwenye mabao 10, Balimi Busungu mwenye mabao 8 wote wanaachwa? Naamini hapa kuna tatizo ambalo lazima kama nchi tuweze kulitatua haraka kwa manufaa ya nchi.
Ndiyo maana nimi nasisitiza kwamba katika suala la uteuzi wa wachezaji wa Stars, hasa msimu huu kumekuwa na matatizo makubwa ambayo hatutakiwi kuyafumbia macho, lazima tuambiane ukweli kama tunahitaji maendeleo ya kweli na nchi iweze kuendelea mbele, kwani sisi Watanzania ndiyo wenye mali.
Mimi niliamini kwamba ujio wa Mart Nooij huenda matatizo ya zaidi ya miaka sita yaliyokuwepo kwenye kikosi cha Stars yangekwisha, lakini imekuwa ni tofauti, kwani yameendelea kuwepo jambo ambalo naanza kupata shaka kuwa huenda makocha hawa wanaokuja kufanya kazi kwenye timu za taifa wanapewa uhuru kupita kiasi.
Uhuru huu ndio wakati mwingine unasababisha kuwepo kwa maamuzi ambayo si sahihi na hayana tija kwenye soka la Tanzania na timu yetu ya taifa kwa ujumla wake, kwani mafanikio tunayohitaji hatuyaoni.
Nadhani kuna sababu sasa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) kuchukua maamuzi magumu na kwamba Mkurugenzi wa Ufundi wa shirikisho hilo lazima awe mkali na kumweleza kocha nini ambacho Watanzania wanakihitaji.
Kwa kumbukumbu zangu ni kwamba, Stars chini ya Nooij imeweza kushinda mechi tatu tu kati ya mechi 14. Mechi ilizoshinda ni dhidi ya Zimbabwe bao 1-0 (kufuzu), dhidi ya Malawi bao 1-0 (kirafiki) na dhidi ya Benin mabao 4-1 (kirafiki), hapa ndipo ninapoona matatizo yanaendelea yale yale ya miaka yote ambayo bado hayajashughulikiwa.
Nilishangaa Kocha Nooij akisema kuwa amewaona wachezaji wote kwenye michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, hili inawezekana ni sawa, mbona wale bora waliofanya vizuri kwenye ligi hatujawaona kwenye kikosi cha Stars? Nadhani haya ni maswali magumu ambayo dawati la ufundi linafaa kuwaambia Watanzania. Lakini mwisho ni kwamba, tatizo la Stars ni kubwa zaidi ya tulionavyo.
IMEANDALIWA NA AHADI KAKORE KUTOKA KWENYE MAKALA YA USEMAVYO UBONGO WA KAKORE.
Showing posts with label Michezo. Show all posts
Showing posts with label Michezo. Show all posts
Wednesday, May 20, 2015
Wednesday, April 22, 2015
Mechi nne kuondoka na watu Simba
NA EZEKIEL TENDWA
WAKATI Simba ikiwa imebakisha michezo minne ikianzia na wa leo dhidi ya Mgambo JKT kumaliza Ligi Kuu Tanzania Bara, wachezaji wa timu hiyo watacheza kwa tahadhari kubwa kuepuka panga la usajili mara Ligi hiyo itakapofikia tamati Mei, mwaka huu.
Simba wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi zao 35, nyuma ya Azam wenye pointi 42, kila timu ikiwa imecheza michezo 22, zikibakiwa na michezo minne kumalizia Ligi hiyo ambapo kila moja ikiapa kushinda michezo yake yote.
Ili Simba wamalize nafasi ya pili, wanatakiwa washinde michezo yao yote minne iliyobaki, ukiwamo dhidi ya Azam FC, huku wakiwaombea Wanalambalamba hao kupoteza angalau michezi mitatu kati ya minne waliyobakiwa nayo.
Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic, ameweka wazi kuwa bado ana matumaini ya kikosi chake kumaliza katika nafasi ya pili, huku akitamba kuibuka na ushindi mnono dhidi ya maafande hao wa Mgambo leo, ili kuzidi kuwasogelea Azam.
Ukiacha mchezo wa leo, Simba imesaliwa na mechi dhidi ya Azam FC, Ndanda FC na JKT Ruvu.
Michezo yote hiyo Simba wataicheza katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, huku wapenzi na mashabiki wao wakiwa na hamu ya kuona kikosi hicho kinashinda michezo hiyo ili kujiweka katika mazingira ya kupata nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa mwakani, huku wakiwaombea mabaya Azam FC.
Habari za uhakika ambazo Dimba Jumatano inazo ni kwamba, baadhi ya wachezaji ambao wamesajiliwa kwa bei kubwa na kushindwa kuonyesha cheche zao wapo kwenye wakati mgumu wa kama wataendelea kuwepo kwenye kikosi hicho msimu ujao au kutemwa.
Wachezaji wa Kimataifa, Danny Sserunkuma pamoja na Simon Sserunkuma wapo kwenye mtihani mgumu, kutokana na kusajiliwa kwa bei kubwa huku wakishindwa kufanya mambo ya kulikuna benchi la ufundi.
Nyota ya Ngassa yazidi kung’aa Afrika
NA SHARIFA MMASI
WAKATI winga wa Yanga, Mrisho Ngassa akiwa amemaliza mkataba wake ndani ya kikosi hicho, nyota yake imezidi kung’aa barani Afrika, baada ya klabu kadhaa kuonyesha kukunwa na kiwango chake, hivyo kuitaka saini yake kwa udi na uvumba.
Awali Ngassa alishafanya mazungumzo na kusaini mkataba wa awali na timu ya Free State ya Afrika Kusini, lakini moja ya timu kubwa ya nchini Qatar pia imeonyesha nia ya kumhitaji kabla ya Etoile du Sahel ya Tunisia nayo kufunguka juu ya mchezaji huyo.
Habari za uhakika ambazo DIMBA Jumatano imezipata zinaeleza kuwa, mbali na timu hizo, pia klabu ya AS Vita ya Congo DRC nayo inahitaji saini ya winga huyo, huku klabu yake, Yanga nao wakihaha kumshawishi kumpa mkataba mpya baada ya kuwafanyia mambo kwenye Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, amekiri Ngassa kumaliza mkataba wake na klabu hiyo na kusema suala la mchezaji huyo kutamaniwa na timu mbalimbali barani Afrika kwa sasa halina nafasi kwao, kwani kila kitu kitawekwa wazi baada ya ligi kumalizika Mei, mwaka huu.
"Ni kweli kwamba Ngassa amemaliza mkataba wake, lakini kama mnavyomwona anaendelea kuichezea Yanga hivyo tunawaomba mashabiki wetu wala wasiwe na wasiwasi juu ya jambo hilo, kwani uongozi wao upo makini," alisema Muro.
Simba yamtengea Msuva Ml. 170
NA SAADA SALIM
KAMATI ya Usajili ya Klabu ya Simba imetenga Sh milioni 170 kwa ajili ya kumnasa winga machachari wa Yanga, Simon Msuva, ili aisaidie timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao.
Taarifa zisizo na shaka zilizolifikia DIMBA Jumatano kutoka kwa kigogo mmoja wa Kamati hiyo zinaeleza kuwa tayari wameshatenga donge hilo kwa ajili ya kumnasa Msuva, ambaye amekuwa na msimu mzuri ndani ya Yanga kutokana na kuwa mwiba mkali wa kucheka na nyavu.
"Suala la Msuva kuja Simba halina ubishi wowote, kwani Kamati inaendelea na harakati za kumnasa winga huyo kwa ajili ya msimu ujao," alisema kigogo huyo na kuongeza: "Dau hilo tulilomtengea tuna uhakika kabisa hawezi kulikataa".
Kwa nyakati tofauti Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kepteni Zacharia Hanspope, amekiri uwepo wa mpango wa kuipa pigo Yanga kwa kumchukua Msuva kwa madai kuwa kiwango chake ni kizuri na pia hata yeye mwenyewe anaipenda Simba, hivyo hawana budi kumrejesha nyumbani.
KAMATI ya Usajili ya Klabu ya Simba imetenga Sh milioni 170 kwa ajili ya kumnasa winga machachari wa Yanga, Simon Msuva, ili aisaidie timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao.
Taarifa zisizo na shaka zilizolifikia DIMBA Jumatano kutoka kwa kigogo mmoja wa Kamati hiyo zinaeleza kuwa tayari wameshatenga donge hilo kwa ajili ya kumnasa Msuva, ambaye amekuwa na msimu mzuri ndani ya Yanga kutokana na kuwa mwiba mkali wa kucheka na nyavu.
"Suala la Msuva kuja Simba halina ubishi wowote, kwani Kamati inaendelea na harakati za kumnasa winga huyo kwa ajili ya msimu ujao," alisema kigogo huyo na kuongeza: "Dau hilo tulilomtengea tuna uhakika kabisa hawezi kulikataa".
Kwa nyakati tofauti Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kepteni Zacharia Hanspope, amekiri uwepo wa mpango wa kuipa pigo Yanga kwa kumchukua Msuva kwa madai kuwa kiwango chake ni kizuri na pia hata yeye mwenyewe anaipenda Simba, hivyo hawana budi kumrejesha nyumbani.
Tuesday, February 3, 2015
Simba yafuata dawa Zanzibar
SAADA AKIDA NA SALMA MPELI
KOCHA wa Simba, Goran Kopunovic, ameziangalia silaha zote ndani ya kikosi chake kinachoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuuomba uongozi umpe muda zaidi ajichimbie na timu kisiwani Zanzibar kwa ajili ya kukipika zaidi kikosi chake.
Goran anaonekana kunogewa na marashi ya Zanzibar yaliyompa ubingwa Kombe la Mapinduzi na ndiyo maana ameamua kukipeleka tena kikosi chake kisiwani humo kwa ajili ya maandalizi ya mechi za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba imekuwa na desturi ya kujichimbia kisiwani humo, hasa inapokabiliwa na mechi ngumu pekee, ikiwemo ya mahasimu wa jadi kisoka, Yanga, lakini sasa Kopunovic amesema kambi ya Zanzibar ndiyo anaamini itampa ubingwa.
Mserbia huyo alianza kazi ya kuinoa Simba Januari Mosi, mwaka huu, kwenye michuano ya Mapinduzi na kuipa taji hilo, akisifia mazingira ya utulivu yalisaidia timu yake kufanya vema.
Habari za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Simba zinaeleza Kopunovic amependekeza timu yake kurejea visiwani Unguja baada ya kupaona ni sehemu tulivu kwake kuweza kuwajenga wachezaji kisaikolojia.
"Unajua kule ndipo alipoanzia kazi, kwani aliikuta timu katika michuano ya Mapinduzi ambapo ameyapenda mazingira ya kule akidai ni sehemu tulivu, hivyo ameuomba uongozi kuhakikisha unawafanyia mpango ili timu iweze kwenda tena kujichimbia huko," kilisema chanzo hicho.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, timu hiyo itakwenda kisiwani humo baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union, utakaopigwa mwishoni mwa wiki hii katika Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.
DIMBA Jumatano lilimtafuta Ofisa Habari wa klabu hiyo, Humphrey Nyasio ili kuzungumzia suala hilo, ambapo hakukubali wala kukataa zaidi ya kusema akili yao yote ipo katika mchezo wao huo dhidi ya Coastal Union, kwani wanahitaji pointi zote tatu.
Akizungumzia kurejea kwa kipa wao namba mbili, Hussein Sharrif 'Cassilas', alisema mwishoni mwa wiki hii anatarajiwa kuungana na wenzake katika mazoezi mara baada ya kumaliza mchezo wao dhidi ya Coastal Union.
"Cassillas tunatarajia atajiunga na wenzake mwishoni mwa wiki hii baada ya kutoka Tanga, suala la beki wa kati, Joseph Owino bado anaendelea na matibabu, kwani aliumia nyonga," alisema Nyasio.
Baadhi ya wachezaji wa Simba wakiwa wanaingia uwanjani.
Yanga yatua kininja Tanga
NA EZEKIEL TENDWA
YANGA iko jijini Tanga ilikokwenda kuvaana na Coastal Union ya huko katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Wanajangwani hao walitua Tanga 'kininja' tangu juzi, kabla ya kutoweka na kwenda mafichoni kukwepa hujuma za wapinzani wao wanaojulikana kwa jina la 'Wagosi wa Kaya'.
Timu hizo zinavaana leo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa katika uwanja wa CCM Mkwakwani.
Kikosi cha timu hiyo kilitua Tanga juzi kwa mbwembwe nyingi na kupokewa kifalme na mashabiki wake, huku msafara wake ukiwa chini ya ulinzi mkali wa magari sita mbele na nyuma.
Msafara wa timu hiyo ulipelekwa moja kwa moja kwenye tawi la klabu hiyo katika mji mdogo wa Pongwe, lililoko umbali wa kilomita 35 kutoka jijini Tanga.
Kwa kutambua inaweza kufanyiwa hujuma na wenyeji wao, Coastal Union, Yanga iliamua kukipeleka mafichoni kikosi katika Hoteli ya Central iliyoko katikati ya jiji hilo, huku makomandoo wa timu hiyo wakilazimika kuweka ulinzi wa kutosha kwa wageni wanaoingia na kutoka.
Itakumbukwa Yanga inacheza na Coastal Union ikiwa ni siku chache ikitoka kukipiga na Ndanda FC na kulazimishwa sare ya bila kufungana, matokeo yaliyowakasirisha mashabiki wa timu hiyo kuhisi pengine inahujumiwa na baadhi ya watu.
Mara baada ya taarifa za Yanga kutua jijini humo kuenea, baadhi ya wadau wa soka, wakiwemo wanazi wa timu hiyo walianza kuisaka kutaka kuwaona baadhi ya wachezaji nyota wa kimataifa kama Mliberia Kpah Sherman, Andrey Coutinho na Amis Tambwe, lakini wakashindwa kujua iliko.
Uchunguzi uliofanywa na DIMBA Jumatano ulibaini mashabiki hao walikuwa na hamu ya kuwaona wachezaji hao ambao Yanga iliwasajili msimu huu, kwani hawajawahi kuwaona isipokuwa Tambwe, ambaye msimu uliopita alikuwa Simba.
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zilieleza uongozi wa klabu hiyo uliamua kufanya mambo yao kwa siri na kuficha uwanja walioutumia kwa mazoezi, ili kukwepa mtego wa wapinzani wao, hali iliyowafanya mashabiki wa timu hiyo kuzidi kuhaha.
Kikosi cha timu hiyo kutokana na uchovu wa safari kilishindwa kufanya mazoezi ambapo benchi la ufundi liliamua programu ya mwisho ya kujifua ingeanza jana jioni kwenye uwanja wa Mkwakwani.
Huu ni mchezo wa kiporo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao unatarajiwa kuwa mkali kwa dakika zote 90, kwani kila timu inahitaji matokeo mazuri ili kujiweka kwenye mazingira mazuri, ikizingatiwa kuwa Ligi yenyewe imefikia patamu.
Yanga wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 19 nyuma ya mabingwa watetezi, Azam FC,waliopo kileleni wakiwa na pointi 21 na kama Wanajangwani hao wataibuka na ushindi watapanda juu na kuwazidi Wanalambalamba hao kwa pointi moja.
Kwa upande wao, Coastal Union wapo nafasi ya sita wakiwa na pointi 17 na kama nao wataibuka na ushindi watapanda hadi nafasi ya pili wakifikisha pointi 20 na kuwaacha nyuma Yanga kwa pointi moja, kitu ambacho kinaufanya mchezo huo kuwa wa shika nikushike.
Yanga chini ya Kocha wao Mkuu, Mholanzi Hans Van Pluijm, itawategemea zaidi mastraika wao mahiri, Tambwe, Sherman na Mrwanda mwenye mabao matano, akizidiwa kwa mabao mawili na Didier Kavumbagu wa Azam mwenye mabao saba na Rashid Mandwa wa Kagera Sugar na Samuel Kamuntu wa JKT Ruvu kila mmoja akiwa na mabao sita.
Hata hivyo, Yanga wasitarajie mteremko, kwani Coastal Union kupitia kwa Msemaji wao, Oscar Asenga, wameapa kula sahani moja na Wanajangwani hao, wakitaka kuhakikisha wanautumia vizuri uwanja wao wa nyumbani na kuibuka na ushindi ili dhamira yao ya kumaliza moja ya nafasi za juu msimu huu itimie.
"Kama watu wanadhani Yanga watakuwa na kazi rahisi wamekosea, hatuwezi kukubali kudondosha pointi tatu, tena kwenye uwanja wetu wa nyumbani, sisi tuna pointi 17 kama tukiwashinda tutakuwa nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 20, vijana wetu wanajua nini tunakitafuta msimu huu," alisema Asenga.
Takwimu zinaonyesha mara ya mwisho Yanga kuifunga Coastal Union ilikuwa ni Novemba 11, 2012, kwenye uwanja wa Mkwakwani, ikishinda 2-0 lakini baada ya hapo timu hizo zimekuwa zikienda sare katika mechi zote zilizofuata.
Mei 18, 2013, timu hizo zilikutana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kwenda sare ya bao 1-1 na kukutana tena Agosti 28, 2014, kwenye uwanja huo na kutoka sare nyingine kama hiyo.
Aidha mechi ya mwisho kuzikutanisha timu hizo ilikuwa ni ile ya Januari 29, mwaka jana jijini Tanga, ambapo timu hizo zilitoka suluhu pia.
Kikosi cha Yanga kikiwa mazoezini.
Friday, July 11, 2014
Tuesday, July 8, 2014
Tuesday, July 1, 2014
Stars yapiga mechi mbili Botswana
TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inatarajiwa kucheza
mechi yua kirafiki dhidi ya Lesotho, Julai 5 mwaka huu ikiwa ni siku moja kabla
ya kurejea nchini Julai 6. Stars ipo Gaborone, Botswana ilikoweka kambi ya wiki mbili
kujiandaa na mechi ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika (AFCON 2015) zitakazofanyika nchini Morocco.
Yanga wakana dau la Ngassa
Marcio Maximo, Kocha wa Yanga
KLABU ya Yanga, imesema kuwa haijapata
ongezeko la dau la kumnunua nyota wao, Mrisho Ngassa kutoka klabu ya Free State
Stars ya Afrika Kusini.
Baada ya kufuzu katika majaribio
hayo, imeelezwa kuwa klabu hiyo ya Afrika Kusini ilituma ofa kwenda Yanga
ambayo ni Doa za kimarekani 80,000 zaidi ya milioni 134 fedha za Kitanzania
ingawa ofa hiyo ilikataliwa kwani Yanga walikuwa kihitaji Dola 150,000, zaidi
ya milioni 250.
Hata hivyo dira ya ulimwengu ilimtafuta
Mwenyekiti wa mashindano wa Yanga ambaye pia mara kadhaa amekuwa akishughulikia
usajili, Seif Ahamed ‘Magari’ alikana kuwa Yanga ilitaka dao hilo la Dola
150,000 ingawa hakutaja kiasi gani kilichopendekezwa.
Friday, June 27, 2014
Monday, June 23, 2014
MIROSLAV CLOSE anatafuta historia ya Kombe la dunia
Klose akishangalia bao.
Alhamisi, michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Brazil itakuwa katika hatua muhimu ambapo itajulikana ni timu zipi zinasonga mbele kuelekea kwenye timu 16 bora na zipi zinatakiwa zikirejea nyumbani. Huku kukiwa na mtu anaitwa Miroslav Klose mshambuliaji wa Ujerumani ambaye anataka kuvunja rekodi ya kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo baada ya kufikisha idadi ya mabao 15 ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na nguli wa soka kutoka Brazil, Ronaldo De Lima.
Subscribe to:
Posts (Atom)





