NA JENNIFER MANONI
RUTH Suka ni mwigizaji wa siku nyingi kutoka katika Kundi la
Kaole Sanaa lililokuwa linatamba miaka ya nyuma na maigizo yake yaliyokuwa
yanaonyeshwa kupitia televisheni ya ITV.
Mwanadada huyo ni miongoni mwa waigizaji wengi wanaofanya
vizuri kwa sasa kwenye tasnia ya filamu Tanzania na Afrika Mashariki na Kati
kwa ujumla.
Miongoni mwa waingizaji hao waliokuwa wanaunda kundi la Kaole
wakati huo ni pamoja na Vicent Kigosi ‘Ray’, Hissan Muya ‘Tino’, Muhsin Awadh
‘Dr Cheni’ Elizabeth Michael ‘Lulu’, Marehemu Steven Kanumba, Blandina Chagula
‘Johari’ na wengine wengi.
Kupitia safu hii Dimba lilipata fursa ya kuzungumza na
mwanadada huyo kwa ajili ya kujua mambo muhimu matano kutoka kwake ambayo
yamekuwa ni sehemu ya mafanikio yake tangu alipoanza maisha yake ya filamu.
UPENDO
“Wasanii kwa sasa hatupendani hata kidogo hadi pale unapotokea
msiba au sherehe ndiyo utawaona wakikaa pamoja na kujifanya wanampenda mtu ila
wakati alipokuwa hai au alipokuwa na matatizo wanaishia kumsema pembeni tu, ila
hii imenifanya kufanya kazi kwa bidii na kujitegemea badala ya kutegemea watu
wengine.
CHANGAMOTO
“Changamoto kubwa katika kazi yangu ni wasanii wengi kutojali
muda wa kufika kwenye eneo la kurekodia ‘location’ na mara kadhaa hii iankuwa
nio tofauti na vile mnavyokubaliana. Mambo haya wakati mwngine najiuliza ni kwa
nini mtu anafanya hivi au kuna nia ya kuniharibia kazi ila ndiyo hali ya watu
ninaofanya nao kazi.
MAISHA YA
WASANII
“Maisha ya wasanii ni mabaya ila wanalazimisha kuishi hivyo
kwa kulazimisha kutokana na majina yao na ndiyo sababu wanajitahidi kubadilisha
nguo na magari ambayo yanakuwa kitendawili kama ni ya kwao au wanayaazima.
Kifupi maisha yao ni ya filamu au maigizo si maisha halisi.
MALENGO
“Kwa sasa nimesimama kwa muda naangalia kwanza soko la filamu
linavyokwenda ili kama nitakuja kutoa filamu iwe na maana na siyo kulazimisha
kutoa kazi nyingi zisizoeleweka. Kutokana na hilo naweza ukajikuta unauza jina
badala ya kutafuta pesa kwa sanaa kwa sasa ni zaidi ya kazi na sio starehe peke
yake na kuwafurahisha tu watu.
STAREHE
“Wasanii
tumeweka starehe mbele kuliko kazi hiyo yote ni kutokana na kuridhika mapema
kwa vijisenti anavyochukua au anavyopata kutokana na kazi husika, hili ni
tatizo ambalo lazima sasa wasanii wenyewe wabadili fikra zao,” anasema nyota
huyo.
No comments:
Post a Comment