Timu Yanga ya Dar es Salaam imeondolewa kwenye michuano ya Afrika baada ya kukubaki kufungwa bao 1-0 na Etoile du Sahel ya Tunisia katika mchezo uliopifanyika kwenye Uwanja wa Olympique de Sousse, uliopo jijini Sousse.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 hivyo kazi kubwa ilibakia kwenye mechi ya marudiano ambayo hata hivyo imetolewa.
Kwa matokeo hayo sasa Yanga itabdidi kusubiri hadi mwakani kwani itakuwa na kazi kubwa kushiriki kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kutwaa ubingwa wa Tanzania hivi karibuni ikiwa na mechi moja mkononi.
No comments:
Post a Comment