Saturday, July 26, 2014
Bukuku apata ajali Dodoma
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba, mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili hapa nchini, Bahati Bukuku amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali mbaya katika eneo la Kongwa, mkoani Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, mwimbaji huyo alipata majeraha makubwa sehemu mbalimbali mwilini na kwamba chanzo cha ajali hiyo kinadhaniwa kuwa ni mwendo kasi.
Chanzo hicho hakijaweza kueleza zaidi kwamba Bukuku alikuwa akielekea ama kutoka mkoani Dodoma na kama ndani ya gari hilo kulikuwamo na abiria wengine.
Pia haikuweza kufahamika mara moja kama mwimbaji huyo alikuwa akiendesha mwenyewe gari hilo, ingawa kilithibishwa ajali hiyo na kwamba Bukuku alijeruhiwa vibaya hasa sehemu ya kiuno.
Endelea kuperuzi blogu hii kwa habari zaidi ya tukio hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment