Kiongozi
maarufu wa mashtaka nchini Argentine amepatikana amefariki ndani ya
nyumba yake mjini Buenos Aires, baada ya kumshutumu Rais Cristina
Fernandez kwa kuzuia uchunguzi wa mashambulio mabaya zaidi ya ugaidi
kuwahi kufanyika nchini humo.
Alikuwa akisimamia uchunguzi kuhusiana na mlipuko katika kituo kimoja cha kijamii kilichokuwa kikisimamiwa na wayahudi mjini Buenos miaka 20 iliyopita ambapo watu watano waliuwawa.
Juma lililopita bwana Nisman alimshutumu Rais Fernandez na wakuu wengine kwa kuzuia uchunguzi huo.