Monday, January 19, 2015

Kiongozi wa mashtaka Argentina auawa

Kiongozi maarufu wa mashtaka nchini Argentine amepatikana amefariki ndani ya nyumba yake mjini Buenos Aires, baada ya kumshutumu Rais Cristina Fernandez kwa kuzuia uchunguzi wa mashambulio mabaya zaidi ya ugaidi kuwahi kufanyika nchini humo.

Alberto Nisman (pichani) alikuwa amepangiwa kutoa maelezo ya kina kwa bunge la taifa hilo.

Alikuwa akisimamia uchunguzi kuhusiana na mlipuko katika kituo kimoja cha kijamii kilichokuwa kikisimamiwa na wayahudi mjini Buenos miaka 20 iliyopita ambapo watu watano waliuwawa.

Juma lililopita bwana Nisman alimshutumu Rais Fernandez na wakuu wengine kwa kuzuia uchunguzi huo.

No comments:

Post a Comment