Tarifa zilizotufikia hivi sasa ni kwamba ule mgomo wa mabasi uliodumu kwa muda siku mbili umemalizika rasmi muda mfupi ulipota baada ya makubaliano ya pande zote zilizokuwa zikivutana.
Kwa sababu hiyo usafiri kwenda mikoani na nchi jirani unatarajia kuendelea kupatikana kama waida ndani ya muda mfupi ujao kutoka sasa.
Aidha kwa upande wa usafiri wa Dar es Salaam usafiri umeanza kurejea kwenye hali yake ya kawaida hivi sasa na kwamba wale waliopo makazini ambao walifika kwa taabu muda wa kurejea watapata ahueni na makali ya nauli yatakuwa yamepungua.
kwa simu mbili mfululizo jana na leo kumekuwa na hali mbaya ya usafiri jambo lililowafanya baadhi ya wakati wa jiji la Dar es Salaam kusafiri kwa tabu na wengine kulazimika kutembea kwa mguu umbali mrefu kutaokana na ukosefu wa huduma za daladala.
No comments:
Post a Comment