Tuesday, July 21, 2015

Kakore ataja vipaombele Saba, Same Magharibi



Waalimu wa shule ya Msingi Masandare katika picha ya pamoja na mtangaza nia, Kakore

 Waalimu wa shule ya Msingi Masandare katika picha ya pamoja na mtangaza nia, Kakore

NA MWANDISHI WETU, SAME

MTANGAZA nia kwenye Jimbo la Same Magharibi, Ahadi Kakore asema kuwa iwapo atapata nafasi ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha kunakuwa na mabadiliko ya kweli na yaharaka katika maeneo saba tofauti.
Akizungumza mjini Same kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Same, Kakore ambaye ni mwandishi wa habari za michezo, amesema kuwa nia yake ni kuona jimbo hilo linafanana na majimbo mengine ya mkoa wa Kilimanjaro ambayo yamepiga hatua katika ameneo mengi tofauti.
Alisema miongoni mwa maeneo ambayo atayasimamia kwa nguvu punde atajkapoingia bungeni ni pamoja na Miundombinu ya barabara, Afya, Maji, Usalama wa raia, kilimo cha umwagiliaji, ufugaji wa kisasa, michezo sanaa na ukuzaji wa vipaji kulingana na dunia ya sasa.
"Nipo tayari kuwatumikia wana Same Magharibi, naamini huu ni wakati wa vijana, mimi ndiye mtu ninayefahamu vyema matatizo ya jimbo letu ambalo kiukweli bado lipo nyuma kwenye maneoe mengi.
"Iwapo nikipata ridhaa ya kuwa mbunge wa Same Magharibi nitahakikisha kuwa maeneo yaliyokwama na yaliyokuwa wanaonekana ni miujiza kutendeka itakuwa kweli kwani kila jambo linawezekana.
"Naamini katika watu ndiyo maana nasisitiza kuwa watu waliopo ninashirikiana nao kulivusha jimbo letu kama Mussa aliovyowavusha wana wa Israel kutoka Misri kwenda nchi ya Ahadi, mimi nipo kwa ajili ya kazi hiyo," alisema Kakore.
Aidha Kakore amesema kwamba katika suyala la elimu litaenda sambamba na maendeleo ya michezo na ukuzaji wa vipaji ambapo yupo kwenye mazungumzo na mamlaka husika ili kuweza kuifanya Shile ya Msingi Masandare iwe moja ya shule za kukuza vipaji jambo nlitakalosaidia pia kupunguza tatizo la utoro hasa kwa jamii za wafugaji.
Jimbo la Same Magharibi kwa sasa linasikiliwa na Mathayo David Mathayo ambaye alishawahi kuwa Waziri wa Mifugo na uvuvi kwenye serikali ya awamu ya nne ambayo inamaliza muda wake mwaka huu.

Tuesday, July 14, 2015

Kakore agombea Ubunge Same Magharibi

NA MSHAMU NGOJWIKE
MHARIRI wa gazeti la DIMBA, Ahadi Kakore ametangaza kugombe Ubunge Jimbo la Same Magharibi, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na jijini Dar es Salaam, Kakore alisema kuwa baada ya kujipima na kutafakari juu  ya matatizo yaliyopo kwenye Jimbo la Same Magharibi ameamua kuwania nafasi hiyo ili kupeleka mbele maendeleo yaliyokwama kwa miaka mingi.

Alisema kuwa Jimbo la Same Magharibi ni miongoni mwa majimbo yenye matatizo mengi ikilinganishwa na maeneo mengine katika mkoa wa Kilimanjaro jambo alilodai kuwa kwa wakati huu anahitaji mtu makini, anayefahamu matizo ya Wanasame lakini mwenye uwezo wa kuyashughulikia kwa uhakika.
“Nimetafakari kwa kina nikajipima nikaona kuwa wakati wa kuwatumikia Wanasame Magharibi umefika na kwa muda mrefu wamekuwa wakihitaji mtu makini na mwenye uwezo wa kuwasaidia wananchi kulingana na matatizo waliyonayo.
“Naelewa Same tangu Uhuru tuna matatizo ya Barabara, Maji, Afya, Mazingira na Michezo mambo ambayo yamekuwa ni kero kwa miaka mingi hivyo zinahitaji mtu makini na kijana ambaye anaweza kusaidia kuyatatua kwa haraka na wakati unaofaa,” alisema Kakore.
Kakore ni mwandishi mkongwe wa habari za michezo kazi ambayo ameifanya kwa zaidi ya miaka 15 ambapo alishafanya kwenye vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya Tanzania.