Tuesday, July 14, 2015

Kakore agombea Ubunge Same Magharibi

NA MSHAMU NGOJWIKE
MHARIRI wa gazeti la DIMBA, Ahadi Kakore ametangaza kugombe Ubunge Jimbo la Same Magharibi, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na jijini Dar es Salaam, Kakore alisema kuwa baada ya kujipima na kutafakari juu  ya matatizo yaliyopo kwenye Jimbo la Same Magharibi ameamua kuwania nafasi hiyo ili kupeleka mbele maendeleo yaliyokwama kwa miaka mingi.

Alisema kuwa Jimbo la Same Magharibi ni miongoni mwa majimbo yenye matatizo mengi ikilinganishwa na maeneo mengine katika mkoa wa Kilimanjaro jambo alilodai kuwa kwa wakati huu anahitaji mtu makini, anayefahamu matizo ya Wanasame lakini mwenye uwezo wa kuyashughulikia kwa uhakika.
“Nimetafakari kwa kina nikajipima nikaona kuwa wakati wa kuwatumikia Wanasame Magharibi umefika na kwa muda mrefu wamekuwa wakihitaji mtu makini na mwenye uwezo wa kuwasaidia wananchi kulingana na matatizo waliyonayo.
“Naelewa Same tangu Uhuru tuna matatizo ya Barabara, Maji, Afya, Mazingira na Michezo mambo ambayo yamekuwa ni kero kwa miaka mingi hivyo zinahitaji mtu makini na kijana ambaye anaweza kusaidia kuyatatua kwa haraka na wakati unaofaa,” alisema Kakore.
Kakore ni mwandishi mkongwe wa habari za michezo kazi ambayo ameifanya kwa zaidi ya miaka 15 ambapo alishafanya kwenye vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya Tanzania.


No comments:

Post a Comment