JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI JESHI LA POLISI TANZANIA PRESS RELEASE 28/07/2014
MAJAMBAZI 10 HATARI WAKAMATWA NA SILAHA/BUNDUKI NANE MMOJA MWANAMKE ANAYEJUA KUTUMIA SMG.
Kamanda Kova
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limefanikiwa kukamata mtandao hatari wa majambazi wapatao kumi (10) mmoja wao akiwa ni mwanamke anayeshiriki kikamilifu wakati wa matukio ya ujambazi. Majambazi hao wamekamatwa katika msako mkali unaoendelea jijini Dar es Salaam katika harakati za kuhakikisha kwamba maisha na mali za wakazi wa Dar es Salaam vinalindwa kikamilifu.
Katika msako huo watuhumiwa walipekuliwa katika miili, makazi, na maficho yao na wakakamatwa na jumla ya silaha 8 kama ifuatavyo.
1. SMG NO. 13975 ikiwa na risasi 11 na magazine 2
2. SMG 1 haikuwa na magazine na namba hazisomeki.
3. BASTOLA 1 aina ya LUGER yenye namba 5533K
4. BASTOLA 1 aina ya BROWNING yenye namba TZACR83494 S/No.7670 Na risasi 6 ndani ya magazine.
5. S/GUN PUMP ACTION na risasi 55
6. MARCK IV iliyokatwa mtutu na kitako yenye magazine 1 na risasi 4
7. BASTOLA 1 yenye namba A963858 browning ambayo ina risasi 1
8. SMG 1 ambayo iko kwa mtaalam wa uchunguzi wa silaha (Balistic)
9. SHOT GUN TZ CAR 86192 ilitelekezwa baada ya msako.
Majina ya watuhumiwa ni ifuatavyo:-
1. MAULIDI S/O SEIF MBWATE miaka 23, mfanyabishara, mkazi wa Mbagala Charambe.
2. FOIBE D/O YOHANES VICENT miaka 30, hana kazi, mkazi wa Mbagara Kibondemaji.
3. VICENT S/O OGOLA KADOGOO miaka 30, mkazi wa Mbagara Kibondemaji
4. SAID S/O FADHIL MLISI miaka 29, dereva wa Bodaboda, Mkazi wa Gongolamboto
5. HEMEDI S/O AWADHI ZAGA miaka 22, dereva wa Bodaboda, mkazi wa Gongolamboto
6. MOHAMED S/O IBRAHIM SAID miaka 31, Fundi welder mkazi wa Kigogo.
7. LUCY MWAFONGO. Miaka 41, mama lishe mkazi wa Vingunguti Ukonga
8. RAJABU S/O BAHATI RAMADHANI, miaka 22, Mkazi wa Kariakoo
9. DEUS JOSIA CHILALA miaka 30, Mgonga Kokoto Kunduchi , mkazi wa Yombo Kilakala.
10. MARIETHA D/O MUSA miaka 18, mkazi wa Yombo Kilalakala Mwanamke pekee katika kundi hilo anayejulikana kwa jina la FOIBE D/O YOHANES VICENT ameshiriki katika matukio ya uporaji wa kutumia silaha, mauaji, n.k. na yeye mwenyewe alikuwa akitumia bunduki aina ya SMG.
Katika baadhi ya matukio wananchi walioshuhudia matukio haya wamekuwa wakitoa taarifa kwamba alikuwepo mwanamke aliyekuwa akifyatua risasi na hatimaye polisi walifanikiwa kumkamata akiwa na wenzake katika kundi hilo.
Licha ya kukamatwa kwa mtandao huu hatari Jeshi la Polisi linaendelea na misako ya mitandao mingine ya ujambazi kwa madhumuni yaliyotajwa hapo juu. Hivyo tunawashukuru wananchi kwa namna walivyoendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutokomeza uhalifu.
Majambazi hao watafikishwa mahakamani baada ya Mwanasheria wa Serikali kupekua majalada yao ya kesi mbali mbali.
MITAMBO NA VING’ORA KATIKA TAWI LA STANBIC BANK KARIAKOO
VYAWAKIMBIZA/KUWAKURUPUSHA MAJAMBAZI KABLA YA KUKAMILISHA DHAMIRA YA KUPORA FEDHA ZA BANK Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limeanzisha msako mkali wa kuwatafuta majambazi watano ambao jana tarehe 27/7/2014 saa 8.00 mchana walifika katika benki ya Stanbic Tawi la Kariakoo lililoko mtaa wa Swahili.
Watatu kati yao waliingia ndani ya benki hiyo wakiwa na mifuko mikubwa wakijifanya ni wateja waliopeleka fedha nyingi katika benki hiyo. Watu hao watatu walipoingia ndani walianza kulazimisha kuvuka wigo wa wateja wa kawaida na kutaka kuingia kwa nguvu kwenda kupora fedha.
Stanbic Bank ina mitambo ya aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na ving’ora vya tahadhari. Ving’ora hivyo vilianza kulia kwa sauti kubwa nje na ndani ya benk hiyo hali iliyowatia kiwewe wahalifu hao.
Waliamua kurudi nje kwa kasi ambapo kulikuwa na gari aina ya Noah na pikipiki moja ambazo hazikusomeka namba kwa haraka na wakatoweka baada ya kufyatua risasi hewani na kuwatisha watu waliokuwa nje na ndani ya Benk.
Baada ya kuondoka majambazi hao iligundulika kwamba mmojawao alichota kwa mkono kiasi cha fedha ambazo mteja alizileta kwa madhumuni ya kuziweka katika Tawi hilo.
Baada ya kutoroka majambazi hao waliterekeza mifuko mikubwa ambayo walitegemea kubebea fedha watakazopora katika benk hiyo ambayo imehifadhiwa kama kielelezo na ndani ya mifuko hiyo waliweka kokoto na uchafu mwingine kwa madhumuni ya kuwadanganya walinzi na watumishi wa benk kwamba walikuwa wamebeba fedha za kuweka benki.
Kutokana na tukio hili tunahimiza benki zote kuchukua tahadhari za kiusalama ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba wanaingia mkataba wa kulindwa na Jeshi la Polisi, kuweka vifaa mbali mbali vya ulinzi vikiwemo ving’ora (alarms), CCTV Camera na mashine za kugundua (metal detectors) mtu anapoingia na silaha au kitu kingine cha hatari kama visu, mitarimbo n.k.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TAHADHARI YA KIUSALAMA KUELEKEA SIKUKUU YA IDD EL HAJI 2014.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeweka mikakati ya mpango kazi kama ifuatavyo:-
Limepanga kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Kampuni binafsi za ulinzi, Vikosi vya uokoaji wakati wa majanga, na vikundi vya Ulinzi Shirikishi ili kuhakikisha kuna udhibiti wa matukio ya uhalifu au fujo zinazoweza kujitokeza.
Tumejipanga kutumia Kikosi cha FFU kikijumuisha askari na magari ya washawasha, Askari wa Mbwa na Farasi. Kikosi cha Polisi Wanamaji nacho kitakuwepo. Pia Vikosi vya Kuzuia Dawa za Kulevya, askari wa kawaida (GD), askari wa Usalama Barabarani, na askari Makachero.
Wote hawa wamepewa maagizo maalum ya kuchukua hatua kabla matukio ya uhalifu hayajajitokeza na sio kungoja tukio lifanyike.
Kwa mantiki hiyo, dalili zozote za uvunjifu wa amani litashughulikiwa pasi na ajizi. Zitakuwepo doria za Miguu, doria za pikipiki na doria za miguu katika barabara zote muhimu.
Wananchi wanashauriwa kusherehekiea siku ya Idd El Haji katika ngazi ya familia au kukusanyika katika mitaa kwa amani wakisherehekea.
1. RPC ILALA: Mary Nzuki – SACP 0754 009 980 / 0754 339 558 2.
2. RPC TEMEKE: Kihenya wa Kihenya – SACP 0715 009 979/ 0754 397 454 3.
3. RPC K’NDONI: Camillius Wambura – ACP 0715 009 976 / 0684 111 111.
“NAWATAKIA NYOTE HERI YA IDD EL FITR
2014”.
S.H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment