UGAIDI HAUNA UHUSIANO NA DINI ASEMA SHEIKH ATAKA VIONGOZI WA DINI ZOTE KUKUTANA NA SERIKALI KUTAFUTA MFADHILI WA UGAIDI NCHINI
|
kaimu sheikh wa mkoa wa
Iringa Abubakar
Chalamila |
|
Waumini wa dini ya kiislamu mjini Iringa wakiwa katika ibada ya idd uwanja wa Samora leo |
|
Ibada ya idd ikiendelea katika uwanja wa Samora mjini Iringa leo
|
|
Waumini wa dini ya kiislam Manispaa ya Iringa wakiswali pamoja ibada ya Idd leo |
|
Waumini wa dini ya Kiislam Iringa wakiwa katika ibada |
|
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza wa tatu kushoto akishiriki ibada ya Idd |
|
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza akiwa na Sheikh Wanguvu kulia mara baada ya ibada ya Idd |
|
Aliyekuwa
mwenyekiti wa UVCCM Iringa mjini Ibrahim Ngwada akiwa na mmoja kati
ya watoto walioshiriki ibada ya Idd wakipongezana kwa kumalizika kwa
mwezi mtukufu |
|
Furaha ya Idd Iringa |
|
Wazee
maarufu na makada wa CCM ambao ni waumini wa dini ya Kiislam
wakipiga picha ya pamoja na mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza
kulia wa pili kulia ni Mr Mbata |
|
katibu mkuu wa watuma salam mkoa wa Iringa Mood Mambo akifurahia jambo baada ya kumalizika kwa swala ya Idd leo |
|
Wadau maarufu wa matukiodaioma Iringa katika picha ya pamoja |
|
Mzee wa matukiodaima wa pili kulia akiwa na wadau wake |
WAKATI
matukio ya uvurugaji wa amani yanayohusishwa na vitendo vya
ugaidi yakiendelea kuota mbawa nchini , kaimu sheikh wa mkoa wa
Iringa Abubakar
Chalamila amewataka
waislamu na viongozi wa dini zote nchini kuendelea kuliombea
Taifa huku akidai kuwa matukio hayo ya ugaidi yanayoendelea hayana
mahusiano na dini yoyote isipo kuwa wapo baadhi ya wana siasa
wanatumia mwanya huo kwa matakwa binafsi ya kuligawa Taifa.
Akizungumza
jana mara baada ya
swala ya Idd iliyofanyika katika uwanja wa Samoraka Sheikh
Chalamila alisema siku zote toka nchi inapata uhuru wake mwaka
1961 dini ya Kiislam na kikristo zilikuwepo na hakukuwa na matukio
ya kigaidi kama yanayojitokeza sasa kwa maparoko na masheikh
kuvamiwa na kumwangiwa tindikali na hata baadhi ya maeneo kutokea
milipuko ya mabomo kama mkoani Arusha na Zanzibar .
Kwani
alisema iwapo kungekuwa na vita za kidini kama zilizo nchi
inyinge duniani kweli akiwa kama kiongozi wa dini angekuwa ni
mtu wa kwanza kuamini kuwa matukio hayo ya kigaidi yanayotokea
yanamahusiano ya karibu na dini ila uongozi wa nchi yetu toka
hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere hadi Rais wetu Jakaya
Kikwete wameendelea kuliunganisha Taifa na kuwa pamoja bila kuwepo
kwa misuguano ya kidini .
"
Sasa kama watanzania tu wamoja kwa muislamu na Mkristo kukaa
pamoja kama ilivyo hivi iweje ugaidi uwepo ......ugaidi kati ya
dini na dini hutokea pale penye tofauti na misuguano ila katika
Taifa letu hakuna misuguano baina ya waislam na wakristo kila mmoja
ana abudu kwa uhuru ....ila wapo watu siwezi kusema moja kwa moja
kama ni wana siasa ama vipi ila wapo wanaotaka kutugawa kwa misingi
ya dini ili kufanikisha
mambo yao ya kisiasa ama ya kiuchumi "
Hivyo
alisema ili kuweza kubaini mbaya wetu anayesababisha machafuko
nchini ni vema viongozi wa dini zote na serikali kukaa meza
moja ili kutafuta mchawi wetu kabla ya kumwacha aendelee kufanya
hivyo kwa iwapo ufumbuzi hautapatikana na mtu huyo
ama watu hao wakifanikiwa kutugawa basi ni wazi nchi itaingia
katika machafuko mabaya zaidi.
"
Nafasi bado tunayo nawaomba viongozi wa serikali watuite viongozi
wa dini ili tukae kwani watu hawa wanataka kutuvuruga kwa
misingi ya kisiasa ama udini .."
Akielezea
kuhusu mwenendo wa Taifa alisema kuwa hali si nzuri kutokana na
watu kukwepa maadili ya Taifa letu na ndio sababu ya majanga mbali
mbali yanaendelea kujitokeza na hivyo kutaka watanzania kurejea
katika maadili ikiwa ni pamoja na viongozi wa dini kuzidi kuhubiri
amani na kuliombea Taifa.
Katika
hatua nyingine Sheikh Chalamila alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa
madai kutoka kwa baadhi ya watu kuwa waislamu si wamoja kutokana
na kutofautiana siku ya kuswali Idd ila ukweli ni kuwa waislam
ni wamoja na wameshikamana isipo kuwa tofauti ya kuanza kufungua
inatokana na matawi katika dini hiyo
kama zilizodini nyingine hivyo si jambo la kuwaona kama hawapo
pamoja.
Picha na habari kwa hisani ya MatukiodaimaBlog
No comments:
Post a Comment