Tuesday, July 1, 2014

Di Maria aibeba Argentina usiku

'Muuaji' waji Di Mario akishangilia

TIMU ya Taifa ya Argentina iliweza kuvuka kwenye hatua ya 16 Bora kwa mbinde baada ya kuifunga Uswiss bao 1-0 katika mechi ngumu kwa kila upande huku bao hilo likifungwa katika muda wa nyingeza.

Mchezo huo uliokuwa wa hatua ya 16 Bora wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu zinazoendelea mchinin Brazil, wakati ambao nchi za Agfrika zikiwa zimeaga michuano hiyo.

Argentina itamshukuru kiongo mshambuliaji, Angel di Maria ambaye katika dakika ya 118 ya mchezo huo aliiwezesha timu yake kupata bao kupata bao baada ya kumaliza dakika 90 kwa matokeo ya 0-0, ambapo mwamuzi Jonas Eriksson raia wa Sweden, kuongeza dakika 30 zilizoibeba Argentina.

Di Maria (26) amabye anakipiga katika kikosi cha Real Madrid ya Hispania alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi kutoka kwa Lionel Messi hali iliyofanya matokeo kusomeka bao 1-0.

Katika mchezo huo ukifanyika kwenye mji wa Sao Paulo,  kila upande ulikuwa ukihangaika kuhakikisha unapata matokeo mazuri ambapo zaidi ya mashabiki 63,255 waliweza kuhudhuria mchezo huo.

Aidha licha ya idadi hiyo ya mashabiki lakini waliwepo wengine zaidi ya 70,000 ambao walifasiri kutoka Argentina hadi Brazil kwa lengo la kuipa nguvu timu yao.

Miongoni mwa mashabiki wa Uswiss ambao walishuhudia mchezo huo ni pamoja na Rais Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Sepp Blatter.

Katika mchezo huo, wachezaji wa Argentina, Rojo,  Booked, Garay Booked na Di Maria wote kutoka Argetina wote walizawadiwa kadi za njano baada ya kuonyesha mchezo mbaya huku Xhaka Booked na Fernandes wa Uswiss wakipewa kadi hizo kutokana na kuonyesha mchezo mbaya.

Kwa matokeo hayo sasa, Argentina itapamba na Ubeligiji ambayo imefuzu kw akuifunga Marekani mabao 2-1 katika mchezo uliokuwa mkugumu kwa pande zote ambao ulimnalizika ndani ya dakika 120.

Furaha





SAO PAULO, BRAZIL

No comments:

Post a Comment