Mwenyekiti
wa Chama cha Wabunge la Jumuiya ya Madola (CPA) tawi la
Tanzania, Mh. Mussa Zungu akizungumza na Katibu wa Bunge,Dk.Thomas
Kashililah(kulia)wakiwa kwenye ziara ya tathmini ya Maandalizi ya
Mkutano wa 45 wa CPA utakaofanyika jijini Arusha mwezi huu,jana
walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara mkoa wa Arusha,kushoto
ni Meneja Uhusiano wa Tanapa, Pascal Shelutete na katikati Mhifadhi Mkuu
wa Hifadhi hiyo, Domician Njau.
Afisa Utalii wa Hifadhi ya Ziwa Manyara, Jully Lyimo(wa pili
kushoto)akiwaongoza Wabunge na Maafisa wa Bunge waliotembelea Hifadhi
hiyo jana.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wabunge la Jumuiya ya Madola (CPA) tawi la Tanzania, Mheshimiwa Mussa Zungu akiwa na Wajumbe wa Bunge hilo na
Maafisa wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwenye Hifadhi ya
Taifa ya Ziwa Manyara hivi karibuni.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wabunge la Jumuiya ya Madola(CPA)tawi la
Tanzania,Mheshimiwa Mussa Zungu(kulia)akizungumza jambo wakati Wajumbe
wa Bunge hilo wakiwa kwenye ziara ya tathmini ya Maandalizi ya Mkutano
wa 45 wa CPA,jana walitembelea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara mkoa wa
Arusha,kushoto ni Wajumbe wa CPA, Beatrice Shelukindo na Mhonga Ruhwanya.
Mwikolojia
wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara,Yustina Kiwango akizungumzia hali
ya Hifadhi hiyo kwa Wajumbe Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola tawi
la Tanzania(CPA)waliotembelea ikiwa ni maandalizi ya Mkutano mkubwa
utakaofanyika mwezi huu jijini Arusha.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Stephano Qolli akitoa taarifa fupi ya Hifadhi hiyo kwa Wajumbe wa Bunge la Jumuiya ya Madola(CPA)tawi la Tanzania wakiwa kwenye ziara ya tathmini ya Maandalizi ya Mkutano wa 45 wa CPA walipotembelea Hifadhi hiyo.
No comments:
Post a Comment