Wednesday, July 2, 2014

Wajasiriamali Saba Saba waonyesha uwezo

Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama maonyesho ya Saba Saba yameendelea kuwa kivutio kwa wananchi wengi wa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam huku wajasiriamali kutoka naeneo mbalimbali wakiwa ni sehemu ya kivutio hicho kutokana na uwezo wao wa kuzalisha bidhaa bora.

Huyu ni Jonesia P John akiwa na bidhaa za asaili ndani ya mbanda la Pride Tanzania kwenye maonyesho hayo.
Bidhaa zenyewe ndiyo hizi hapa.


Mrs Chacha naye alikuwepo kwneye maonyesho ya mwaka huu akiwa na bidhaa zake za mikoni ambazo ni pamoja na mashuka, vitambaa vya meza na mambo mengine mazuri ya nyumbani.


PAMOJA NA KUWEPO KWA WAJASIRIAMALI WENGU ILA HAWA KUTOKA ZANZIBAR NAO WAMEPAMBA VILIVYO MAONYESHO YA MWAKA HUU

Bi. Mwanakhamis M. Pazi ambaye ni Mkurugenzi wa Mwani Designer of Coconut Product (MDCP) akiwa na mshirika mwenzake kwenye maonyesho hayo ambaye naye anatoka katika Taasisi hiyo wakionyesha bidhaa wanazozalisha.  
 

Bidhaa kutoka Zanzibar.

KUTOKA MOSHI MKOANI KILIMANJARO TUNAKUTANA NA MAMA GRACE MURO

Huyu ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa G.M Food Products, Bi. Gece Muro akionyesha bidhaa ambazo kampuni yake inazalisha. 

Baadhi ya bidhaa ambazo zinazalioshwa na kampuni hiyo ni pamoja na vinywaji ikiwemo vya soya pia inajihusisha na kukausha mbogamboga na matunda. Picha zote na www.dirayaulimwengu.blogspot.com 

  

No comments:

Post a Comment