Thursday, July 3, 2014

Balozi wa Libya ajiua Dar

Balozi wa Libya nchini Tanzania amejiua kwa kujipiga risasi kichwani. Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam , John Solombi anasema kuwa balozi huyo kwa jina Ismail Nwairat, alijipiga risasi Jumanne usiku na kufariki akiwa anapokea matibabu hospitalini.
Msemaji wa serikali ya Tanzania Arthur Mwambene amethibitisha taarifa hiyo kuwa balozi huyo alijiua ndani ya makao ya ubalozi wa Libya mjini Dar es Salaam Jumanne usiku.
hadi sasa hakuna taarifa zozote zilizotolewa juu ya suala hilo na kwamba Polisi wanaendelea na ujuchunguzi wa suala hilo.
 Bendera ya Libya

No comments:

Post a Comment