Wednesday, August 13, 2014

Hapa ndipo Cecafa ilipochemka



JUMAPILI iliyopita katika gazeti la DIMBA nilizumzia suala lilaloendelea kutokota Afrika Mashariki na Kati hasa baada ya Yanga kuenguliwa kwenye michuano ya Kombe la Kagame mwaka huu.
Wapo ambao walinipinga na wengine waliniunga mkono, binafasi niwapongeze wote na kuwashukuru kwani wameonyesha ukomavu wa hali ya juu wa kupembua mambo.
Lakini kutokana na unyeti wenyewe na uzalendo wangu kwa Tanzania, nimeamua kuamalizia baadhi ya mambo niliyoona yanastahili kufafanuliwa ili jambo hili liweze kueleka sawa.
Pia kuepusha baadhi ya watu kutowafanya Watanzania kisima cha fedha au ghala la fedha, kama wanavyotaka kufanya baadhi ya viongozi wa Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).
Mfano kwenye Kombe la Kagame msimu huu Yanga iliondolewa Cecafa kwa madai ya kupeleka wachezaji wa timu B badala ya A. Hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya msingi ambayo Cecafa kupitia Katibu Mkuu wake Nicholas Musonye iliueleza umma wa wapenda soka Afrika Mashariki na Kati kwamba suala la timu B ndiyo dhambi kubwa iliyoigharimu Yanga.
Awali niunga mkono maamuzi ya Cecafa lakini baada ya kufanya utafiti wa kina niliweza kugundua makosa na udhaifu mkubwa katika jambo hili ingawa suala la kipato ndilo lililochukua nafasi kubwa badala ya kweli wa mambo kwa liugha rahisi ni kwamba Cecafa haikusema kweli.
Kama Yanga ingekwenda singekuwa timu pekee iliyopeleka wachezaji vijana ila timu zilichukua hatua hiyo ni nyingi lakini kutokana na umaarufu wa timu za Tanzania hasa Simba na Yanga ndiyo nongwa ilianzia hapo.
Kwa mfano katika michuano ya mwaka huu kuna klabu ya Ethiopia iitwayo Adama City Oromiya FC ‘Nazareth’ ambayo ilipeleka vijana, hivyo kwa uelewa wa kawaida tu ni kwamba kuna tatizo kwenye suala la kuchukuliwa kwa maamuzi haya kwani mbona Adama City haikuondolewa?.
Najiuliza je? hawa Adama City wachezaji wao wa timu B ni tofauti gani na wale wa kikosi B cha Yanga. Ndiyo maana nasema katika jambo hili Cecafa ilikosea au ilichemka kama wasemavyo vijana wa kizazi cha sasa.
Ili kuonekana kuwa Cecafa ilipotea njia ni kwamba kanuni zake za wachezaji wanaotakiwa kucheza kwenye michuano ya Kagame, wanatakiwa wenye leseni ya shirikisho la nchi kusika yaani kama ni timu kutoka Tanzania lazima mchezaji awe na leseni kutoka shirikisho la soka la nchi husika.
Nilifikiri kwa sababu Cecafa haina michuano yoyote ya umri ingeona fahari kuwatumia vijana zaidi ili kuwasaidia ikiwemo kutoka katika nchi zao na kwenda kwenye nchi nyingine ndani na nje ya ukanda huu badala ya kuendelea kuwa na mawazo ya kizamani ya kuwategemea wachezaji wale wale.
Kwa hiyo Yanga haikukosea kwa lolote na ilikuwa na haki ya kuamua imtumia nani na imuache nani kwenye michuano ya mwaka huu kwani hata hakuna kanuni inayoibana juu ya kuwatumia wachezaji wa aina gani, kwa lugha rahisi naweza kusema baraza hili linapiga siasa badala ya kufanya maendeleo.
Sasa Cecafa ilitakiwa iwaeleze wadau wa soka kwamba wachezaji wa Yanga waliokuwa wapelekwe kwenye michuano hiyo hawakuwa na leseni ya TFF jambo ambalo si kweli ila walikuwa wameangalia zaidi fedha zinatakazopatikana kutokana na viingilio kwani wangekuwepo akina Mbuyu Twite na wenzake mashabiki wangeongezeka mara dufu.
Ndiyo maana nasisitiza kwamba jambo hili limechukuliwa kwa hasira na kukurupuka tofauti na ukweli ulivyo.
Kwa mazingira haya naendelea kusimamia msimamo wangu kwamba Cecafa ilikosea na ilifanya maamuuzi ya kukurupuka kwani hata leo ukiwauliza kwamba wanaijua ‘first eleven’ ya Azam FC iliyochukua nafasi ya Yanga, au Adama ya Ethiopia ni wazi kwamba hawazijui ila kwa sababu ya umaarufu ya wachezaji wa Yanga ndiyo waliouangalia.

Mwenendo huu wa Cecafa naamini unastahili kubadilika hasa kutokana na umri wake kwenye masuala ya kuendeleza soka Afrika kwa sababu hadi leo baraza hili limeshafikisha umri wa miaka 88.
Kwa umri huu nilitegemea soka la Afrika Mashariki na Kati lingevuka kutoka hapa na kwenda mbele ila imekuwa kinyume kwani maendeleo yake ni madogo na hafifu ikilinganishwa na kanda nyingine.
Kwenye ulimwengu wa sasa suala la uweledi na ukweli ndiyo unaweza kuleta tija na maendeleo lakini kutokana na aina ya viongozi tuliokuwa nao hatuwezi kufika popote kwani wengi wao si wakweli katika utendaji wao.
Kama kweli ukanda huu na Cecafa tunahitaji kufanikiwa lazima badaliko ya kiutendaji yafanyike vinginevyo tunaishia katika soka la wahapahapa na kuziacha nchi nyingine kuendelea mbele.
Pia Cecafa inastahili sasa kuangalia namna ya kupata wadhamini wa mashindano yao badala ya kutegemea viingilio kutoka kwa timu za Tanzania ambazo hasa Simba na Yanga ambazo zimeonekana kuwa na mvuto kwa mashabiki tofauti na timu nyingine za ukanda huu.
Hili likifanyika tunaweza kufanikiwa na kupiga hatua kwani kutakuwa na mfumo bora wa kurithisha vipaji kutoka kikazi kimoja khadi kingine badala ya kuendelea kuwategemea wachezaji wale wale wa miaka yote.
Kama Cecafa itakuwa ikiwategemea Juma Kaseja, Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima na wengineo ili kuendesha michuano yao itakuwa ni hatua ya juu ya kushindwa badala ya kushinda. 

Mwandishi wa makala haya ni Ahadi Kakore-0784890387

No comments:

Post a Comment