Wednesday, August 13, 2014

Simba itatisha tu-Kiongera



NA SAADA AKIDA
KOMBINESHENI ya Mastraika wawili wa Kimataifa wa Simba, Paul Raphael Muigai Kiongera na Amis Tambwe imelikuna benchi la ufundi la timu hiyo lililokuwa likiongozwa na Zdravko Logarusic kabla ya kufukuzwa Jumapili iliyopita.
Awali klabu hiyo ilikuwa inamtegemea Tambwe pekee katika safu ya ushambuliaji ambapo alimaliza msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara akiibuka mfungaji bora kwa kufunga mabao 19.
Breaking News lilishawishika kufanya mahojiano na mshambuliaji huyo raia wa Kenya ambapo katika mazingumzo hayo aliweza kueleza mambo mambalimbali ambayo anaamini yamemfanya kuwemo kwenye kikosi cha Simba msimu huu.
USAJILI WAKE SIMBA:
Kiongera aliyekuwa anakipinga KCB inayoshiriki Ligi Kuu Nchini Kenya anasema alitoa kwa maa ya kwanza ndani ya Simba ilikuwa kwa ajili ya mazungumzo na kurejea Kenya kwa ajili ya kuchukuwa kibali katika klabu yake ya zamani ya KCB FC.
 “Nipo Simba kwa muda wa miaka miwili baada ya kumalizika taratibu zote hivyo kwa sasa nitakuwa nikifabya kazi Tanzania,” anasema nyota huyo.
NINI ATAKACHOKIFANYA:
Anasema anachohakikisha ni kutoa ushirikiano mzuri na wachezaji wenzake kufikia malengo ya na matakwa ya timu ambayo ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
“Nimekuja kufanya kazi Simba, moja ya vitu ambavyo nahitajika ni kuhakikisha tunafanya vizuri kwa kupata ushindi, hasa katika ligi ambapo ndiyo kielelezo cha mafanikio kuelekea kwenye mashindanio makubwa ya kimataifa,” anasema.
UPACHA WAKE NA TAMBWE:
 “Unajua nimejiunga siku moja kabla ya mchezo huu (dhidi ya Zesco), kwa hiyo ilikuwa ngumu kuelewana haraka na Tambwe lakini niliweza kumsoma na kumjua haraka jinsi gani natakiwa kumtumia vizuri, naamini kama tukuenda kwa mwendo huu tunaweza kufanya makubwa siku zijazo,” anasema.
Kiongera anasema Tambwe ni mchezaji mzuri jamboa ambalo linampa matumaini ya kufanya vizuri kwa siku zijazo ndani ya kikosi hicho ambacho chenye maskani yake mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.


 


No comments:

Post a Comment