Mcheza filamu wa Kibongo, Kajala Masanja amejeruhiwa vibaya usoni kwa chupa baada ya kupigwa na mtu mmoja ambaye hakujulikana jina lake mara moja na sasa amefikishwa kituo cha Polisi Oystabay jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili usiku kwenye ukumbi wa Maisha Club ambapo baada ya shoo ya Mabesta ambapo baada ya shoo kumalizika kajala na timu yake walikuwa wakielekea nyumbani ambapo jamaa mmoja alikwenda kupiga chupa usoni ambapo alipelekwa hospitali ya mwananyama na kutibiwa kisha kuruhusiwa.
Katika hilo pia alikuwepo pia mkuu wa wilaya ya Kinondini , Paul Makonda ambapo alikuwa ni miongoni mwa watu waliomsaidia Kajala kupata huduma ya kwanza na sasa jamaa husika yupo mikoni mwa polisi.
No comments:
Post a Comment