Tuesday, May 12, 2015

Mnigeria Jodie kuwasha moto Dar

 
Mwanamuziki nyota wa Nigeria, Jodie anatarajiwa kuongoza zaidi ya wanamuziki 30 katika tamasha kubwa la sanaa na utamaduni la Afrika Mashariki  liitwalo Swahili Arts and Creative Carnival litakalofanyika jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa tamasha hilo, Ahadi Kakore amesema kuwa maandalizi yanaendelea vyema ambapo tamasha la mwaka huu litafanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam  na itajywa nara ya kwanza kufanyika kwenye Wilaya ya Temeke.
Kakore alisema kuwa msanii huyo mkali wa wimbo wa  Oooh Baby na nyingine nyingi ameshakamilisha mipango yote kwa ajili ya kuja kufanya shoo hiyo kubwa.
"Kimsingi kila kitu kimekamilika ambapo pamoja na Jodie lakini watakuwepo wasanii wengine wa Afrika Mashariki ambao ni kutoka nchi za Kenya, Uganda na Burundi ingawa idadi kubwa ikiwa ni wasanii kutoka Tanzania ambao ndiyo wenyeji wa shoo hiyo," alisema Kakore.
Tamasha la Swahili Arts and Creative Carnival linafanyika Tanzania kwa msimu wa tatu sasa ambapo mwaka huu limeboreshwa na kuwekewa mazingira bora zaidi tofauti na misimu mingine iliyopita.

 

No comments:

Post a Comment