Wednesday, June 24, 2015
Muuaji wa Stars awaita Simba Taifa
NA MWANDISHI WETU
STRAIKA Mganda, Erisa Ssekisambu ambaye ndiye aliyeifunga mabao 2 kati ya 3 yaliyoitoa Taifa Stars katika mbio za kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan), amewataka matajiri wa Simba, kufika kwenye Uwanja wa taifa kushuhudia muziki wake.
Mganda huyo anayekipiga katika klabu ya SC Villa atakuwepo jijini Dar es Salaam akiambatana na timu yake inayokuja kucheza mechi ya tamasha maalum la kuzuia Mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) Jumamosi katika Uwanja wa Taifa.
Ssekisambu amewaalika Simba baada ya kupata taarifa kwamba viongozi wa timu hiyo wameanza mbio za kusaka saini yake, ikiwa ni siku chache baada ya Shirikisho la soka nchini TFF kuridhia kuongeza idadi ya wachezaji wa kigeni kutoka watano hadi saba.
Akizungumza na toka nchini Uganda, Ssekisambu alisema endapo Simba watafika uwanjani na kuridhishwa na kiwango chake na pia watafikia makubaliano na viongozi wake basi hatokuwa na kikwazo cha kuvaa jezi nyekundu msimu huu na kuungana na Mganda mwenzake Emmanuel Okwi anayekipiga Simba.
Simba imo katika mawindo ya wachezaji watakaokiimarisha kikosi chake, ambapo juzi Rais wa klabu hiyo Evans Aveva alisema wanataka kufanya mapinduzi makubwa ya soka msimu huu kwa kusajili wachezaji wazuri na wenye uwezo watakaoirudishia ubingwa timu hiyo ya Msimbazi.
Msimu uliopita Simba haikufanya vizuri katika michuano ya Ligi Kuu ambapo licha ya kusajili nyota watano wa nje lakini ilishindwa kufurukuta na kujikuta ikimaliza ligi hiyo ikishika nafasi ya tatu.
usemavyo ubongo wa Kakore: Nooij alijifukuza kabla ya kufukuzwa
KOCHA wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’
aliyefukuzwa, Mart Nooij, ni miongoni mwa watu waliopewa kipaumbele kwenye
vyombo vya habari nchini Tanzania kwa muda wa wiki mbili ingawa kwa wiki
iliyopita na mwanzoni mwa wiki hii nguvu hiyo iliongezeka.
Sababu za kupewa nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari
na midomoni mwa wapenzi na mashabiki wa soka la Tanzania, ni kutokana na Taifa
Stars kufanya vibaya katika mechi tano mfululizo jambo ambalo halikuwa la
kawaida kwa muda wote wa zaidi ya miaka 50 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kiukweli kocha huyu inawezekana alikuwa bora lakini
kwa mwelekeo wa soka letu na mfumo wa soka letu alikuwa haendani nao, kwa
kifupi ni kwamba, viatu alivyokuwa amevivaa vilikuwa havukumtosha.
Lakini jambo kubwa ambalo nililiona kwa Nooij, ni
kukosa hamasa na ukaribu na wenye timu yao yaani Watanzania wenyewe, ndiyo
sababu timu ilikosa hamasa kama
ilivyokuwa wakati wa Marcio Maximo na waliokuja baada yake; Jan Poulsen na Kim
Poulsen.
Kosa hili lilikuwa wazi kwani Nooij alisahau kuwa
Stars ni timu ya umma jambo lililomfanya kuiweka timu mbali na wenye timu, hili
ndilo lilikuwa kosa la kwanza kwani hata alipokosea kidogo kwenye uwanja mashabiki
hao walikuwa wa kwanza kumlaumu na kumkosoa.
Makosa ya aina hii hakuna kocha anayeweza kudumu
kwenye timu za taifa kwani ninachofahamu mimi ni kwamba, moja ya sifa ya kocha
wa timu ya taifa ni kuhakikisha inakuwa ni mali ya watu na si mali ya mtu.
Jambo lingine ni kushindwa kuwatumia makocha wazawa
kwa ufasaha, hili limekuwa ni tatizo kubwa kwa makocha wengi wa kigeni
wanaokuja kufanya kazi ingawa wale wanaowatumia wazawa wamekuwa wakifanikiwa.
Kwa mfano, Maximo aliweza kuwatumia makocha kama
Juma Pondamali, Ally Bushiri, marehemu Sylverster Mash, ambao walikuwa
wakilifahamu vyema soka la Tanzania kwani wamekuwa ni sehemu ya soka hilo.
Lakini angalia makocha waliokuja kwenye ngazi za
klabu akiwemo Patrick Phiri alikuwa na wasaidizi wazawa akiwa na kikosi cha
Simba na hata kocha wa sasa wa Yanga, Hans van der Pluijm pamoja na mafanikio
yake ndani ya timu hiyo, amekuwa akitegemea uwepo wa makocha, Charles Mkwassa
na kocha wa makipa, Juma Pondamali.
Mfumo huu ndio umewafanya makocha wengi duniani
kufanikiwa, lakini ilikuwa kinyume kwa Nooij ambaye alikuwa akiamini katika
kile anachokifahamu na naamini alikuwa hashauriwi vyema na wale waliokuwa
wakimsaidia.
Hivyo kwa Nooij naye alitakiwa kuangalia mbali au
kama wanavyosema vijana wa siku hizi alitakiwa kujiongeza zaidi na kuangalia
mbali kwa kushirikisha katika kazi zake makocha wazalendo, lakini nasikitika
kuwa pamoja na wingi wa makocha bora hawajatumika inavyostahili.
Hili limekuwa ni kosa ambalo limemgharimu Nooij na
iwapo akija kocha mwingine kutoka nje ya Tanzania akipewa jukumu hilo kwa siku
za baadaye lazima aambiwe ukweli wa jambo hili kwa maana akidharau atashindwa
tena.
Lakini mwisho wa yote ni kwamba, lazima tukubaliane
kuwa nchi yetu inahitaji kubadilisha mfumo wa soka na uendeshaji wake kwani
bado tupo kwenye mfumo wa kizamani ambao hauwezi kutuvusha.
Miongoni mwake ni pamoja na kuimarisha soka la
vijana na watoto kwani ndiko kwenye mtaji na maendeleo kwa soka letu na si
jambo lingine lolote.
Hapa ndipo tulipokosea, lakini nikiangalia makocha
wapo na wanaweza kutuvusha ila lazima tukubaliane kuwa hawa hawajatumika
ipasavyo na kama likifanikiwa hili tunaweza kusogea mbele lakini si kwa aina ya
kocha kama Nooij kutokana na msimamo wake na aina ya utendaji wake wa kazi.
Kwa sababu hiyo, ninachokiona ni kwamba, Nooij
alijifukuza kabla ya kufukuzwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kwa kushindwa
kuangalia alama za nyakati na wale waliomzunguka na kufanya naye kazi.
Saturday, June 20, 2015
hii ndiyo ratiba ya Ligi ya England
Agosti 8, 2015
Arsenal v West Ham
Bournemouth v Aston Villa
Chelsea v Swansea
Everton v Watford
Leicester v Sunderland
Man United v Tottenham
Newcastle Utd v Southampton
Norwich v Crystal Palace
Stoke City v Liverpool
West Brom v Manchester City
Agosti 15, 2015
Aston Villa v Man United
Crystal Palace v Arsenal
Liverpool v Bournemouth
Man City v Chelsea
Southampton v Everton
Sunderland v Norwich
Swansea v Newcastle Utd
Tottenham v Stoke City
Watford v West Brom
West Ham v Leicester
Agosti, 22, 2015
Arsenal v Liverpool
Crystal Palace v Aston Villa
Everton v Man City
Leicester v Tottenham
Man United v Newcastle Utd
Norwich v Stoke City
Sunderland v Swansea
Watford v Southampton
West Brom v Chelsea
West Ham v Bournemouth
Agosti 29, 2015
Aston Villa v Sunderland
Bournemouth v Leicester
Chelsea v Crystal Palace
Liverpool v West Ham
Man City v Watford
Newcastle Utd v Arsenal
Southampton v Norwich
Stoke City v West Brom
Swansea v Man United
Tottenham v Everton
Septemba 12, 2015
Arsenal v Stoke City
Crystal Palace v Man City
Everton v Chelsea
Leicester v Aston Villa
Man United v Liverpool
Norwich v Bournemouth
Sunderland v Tottenham
Watford v Swansea
West Brom v Southampton
West Ham v Newcastle Utd
Septemba 19, 2015
Aston Villa v West Brom
Bournemouth v Sunderland
Chelsea v Arsenal
Liverpool v Norwich
Man City v West Ham
Newcastle Utd v Watford
Southampton v Man United
Stoke City v Leicester
Swansea v Everton
Tottenham v Crystal Palace
Septemba 26, 2015
Leicester v Arsenal
Liverpool v Aston Villa
Man United v Sunderland
Newcastle Utd v Chelsea
Southampton v Swansea
Stoke City v Bournemouth
Tottenham v Man City
Watford v Crystal Palace
West Brom v Everton
West Ham v Norwich
Oktoba 3, 2015
Arsenal v Man United
Aston Villa v Stoke City
Bournemouth v Watford
Chelsea v Southampton
Crystal Palace v West Brom
Everton v Liverpool
Man City v Newcastle Utd
Norwich v Leicester
Sunderland v West Ham
Swansea v Tottenham
Oktoba 17, 2015
Chelsea v Aston Villa
Crystal Palace v West Ham
Everton v Man United
Man City v Bournemouth
Newcastle Utd v Norwich
Southampton v Leicester
Swansea v Stoke City
Tottenham v Liverpool
Watford v Arsenal
West Brom v Sunderland
Oktoba 24, 2015
Arsenal v Everton
Aston Villa v Swansea
Bournemouth v Tottenham
Leicester v Crystal Palace
Liverpool v Southampton
Man United v Man City
Norwich v West Brom
Stoke City v Watford
Sunderland v Newcastle Utd
West Ham v Chelsea
Oktoba 31, 2015
Chelsea v Liverpool
Crystal Palace v Man United
Everton v Sunderland
Man City v Norwich
Newcastle Utd v Stoke City
Southampton v Bournemouth
Swansea v Arsenal
Tottenham v Aston Villa
Watford v West Ham
West Brom v Leicester
Novemba 7, 2015
Arsenal v Tottenham
Aston Villa v Man City
Bournemouth v Newcastle Utd
Leicester v Watford
Liverpool v Crystal Palace
Man United v West Brom
Norwich v Swansea
Stoke City v Chelsea
Sunderland v Southampton
West Ham v Everton
Novemba 21, 2015
Chelsea v Norwich
Crystal Palace v Sunderland
Everton v Aston Villa
Man City v Liverpool
Newcastle Utd v Leicester
Southampton v Stoke City
Swansea v Bournemouth
Tottenham v West Ham
Watford v Man United
West Brom v Arsenal
Novemba 27, 2015
Aston Villa v Watford
Bournemouth v Everton
Crystal Palace v Newcastle Utd
Leicester v Man United
Liverpool v Swansea
Man City v Southampton
Norwich v Arsenal
Sunderland v Stoke City
Tottenham v Chelsea
West Ham v West Brom
Desemba 5, 2015
Arsenal v Sunderland
Chelsea v Bournemouth
Everton v Crystal Palace
Man United v West Ham
Newcastle Utd v Liverpool
Southampton v Aston Villa
Stoke City v Man City
Swansea v Leicester
Watford v Norwich
West Brom v Tottenham
Desemba 12, 2015
Aston Villa v Arsenal
Bournemouth v Man United
Crystal Palace v Southampton
Leicester v Chelsea
Liverpool v West Brom
Man City v Swansea
Norwich v Everton
Sunderland v Watford
Tottenham v Newcastle Utd
West Ham v Stoke City
Subscribe to:
Posts (Atom)