Wednesday, March 30, 2016
Kiungo Simba aitahadharisha Yanga
NA ZAINAB IDDY
KIUNGO wa zamani wa Simba, Pierre Kwizera, amesikia kuwa Yanga watakabiliana na Al Ahly ya Misri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na sasa ameamua kuwapa somo kwamba wanatakiwa waingie kwa tahadhari kubwa.
Kwizera ambaye kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Rayon Sports ya nchini Rwanda, amesema kama kweli Yanga wana nia ya kufanya vizuri dhidi ya Al Ahly ni lazima wajipange kisawasawa kukabiliana na mbinu chafu za ndani na nje ya uwanja.
“Ukikutana na timu za Kiarabu unatakiwa uwe fiti kuanzia akili kwani jamaa wanajua kutumia viwanja vyao vya nyumbani tofauti na ukanda wetu wa Afrika Mashariki na Kati.
“Kama kweli Yanga wana nia ya kuwatoa lazima wahakikishe wanaibuka na ushindi usiopungua angalau mabao 4-0, kwani vinginevyo itawawia vigumu watakapokwenda Misri wakiwa ugenini,” alisema Kwizera.
Mchezo wa Yanga dhidi ya Al Ahly unatarajia kuchezwa Aprili 9 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, huku ule wa marudiano ukitaraji kuchezwa Aprili 19 nchini Misri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment