Friday, June 27, 2014

Coutinho atua Yanga

Andrey Coutinho

Kiungo mshambuliaji wa Yanga kutoka nchini Brazil, Andrey Coutinho ametua nchini tarai kuanzia kazi. Ujilio wa nyota huyo unakamilisha usajili wa Yanga ambao msimu huu huenda ukawa moja ya klabu tishio kwenye Ligi kuu Tanzania Bara.

Monday, June 23, 2014

20 wauwawa Kenya

 Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Taarifa ambazo zimetufikia ni kwamba zaidi ya watu 20 wameuwa nchini Kenya katika mapiganio ya kikabila na si shambulio la kujitoa mhanga kama ambavyo tulieleza hapo awali. Taarifa kutoka Kenya zinaeleza kwamba tukio hilo lilitokea kwenye  eneo la Wajir nchini.

MIROSLAV CLOSE anatafuta historia ya Kombe la dunia


Klose akishangalia bao.


Alhamisi, michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Brazil itakuwa katika hatua muhimu ambapo itajulikana ni timu zipi zinasonga mbele kuelekea kwenye timu 16 bora na zipi zinatakiwa zikirejea nyumbani. Huku kukiwa na  mtu anaitwa Miroslav Klose mshambuliaji wa Ujerumani ambaye anataka kuvunja rekodi ya kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo baada ya kufikisha idadi ya mabao 15 ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na nguli wa soka kutoka Brazil, Ronaldo De Lima.

Sunday, June 22, 2014

Kutoka Mjengoni : Sitta awahakikishia Watanzania kupata katiba ya kuwalinda wannyonge


Dodoma. Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amechaguliwa kwa kishindo kuliongoza Bunge Maalumu la Katiba, huku akisema kuchaguliwa kwake ni sawa na kumrudisha chura kwenye dimbwi la maji.
Jana, Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), alipata kura 487 na kumbwaga mpinzani wake, Hashimu Rungwe wa Chama cha Ukombozi wa Umma aliyepata kura 69.