Thursday, July 3, 2014

Chuji aibukia Azam FC



KIUNGO wa zzamani wa Yanga, Athumani Iddi ‘Chuji’ (pichani)
ameonekana akiwa na kikosi cha Azam FC akijifua kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hata hivyo bado hapajawa na taarifa zozote za uhakika za Chuji kusajiliwa Azam ila kwa sasa anafanya mazoezi pamoja na kikosi cha Azam ambacho kinajindaa kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita.
Katika siku za karibuni, Chuji amekuwa hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga hasa baada ya kusajiliwa Frank Domayo ambaye amesajiliwa na Azam katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya Kimataifa.
Hivi sasa, Yanga ina viongo wawili matata ambao ni Countinho kutoka nchini Brazil pamoja na Haruna Niyonzima raia wa Rwanda ambao kwa sasa safu ya kiungo itakuwa imeimarika kwa kiasi kikubwa.
Yanga ambayo msimu uliopita ilishikilia nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Tanzania nayo inajiandaa na ligi hiyo huku ikiwa imewatema nyota 11 akiwemo Chuji pamoja na David Luhende.
Naye Kocha wa Azam raia wa Cameroon, Josep Omog amesema kuwa suala la usajili wa Chuji lipo mikononi mwake kwani yeye ni miongoni mwa wakocha wanaoamiani katika kufanya na wachezaji wenye uezoefu hasa kwenye michuano ya kimataifa ambayo imekuwa na changamoto kubwa.

No comments:

Post a Comment