KWELI, Kocha Marcio Maximo anatisha!, hii ni kutokana na mipango yake ya kuifundisha Yanga katika miaka yake miwili kuanzia sasa ambapo kazi hiyo itaanza rasmi leo kwenye viwanja vya bandari huku suala la vipimo likiwa ni la kwanza kufanyika.
Taarifa kutoka ndani ya kikosi hicho zimeeleza kwamba, Yanga inatarajia
kuanza mazoezi hayo chini ya Maximo ambaye itakuwa ni mara yake ya kwanza
kuifiundisha timu hiyo baada ya kumaliza kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya
Tanzania Taifa Stars.
“Kikosi cha Yanga kesho kinatarajia kuanza mazoezi yake chini ya Maximo
katika viwanja vya Bandari Tandika jijini Dar es Salaam ambapo atakutana na
wachezaji wote ambao hawana majukumu ya timu za taifa.
“Miongoni mwa mambo ambayo yatachukua nafasi kubwa ni kupimwa kwa
wachezaji wote ili kujua hali zao za afya, pumzi zao ili kujua wapi pa kuanzia
kwa lengo la kushughulikia maeneo yenye
matatizo kwa wachezaji mmoja mmoja.
“Nadhani itakuwa ni siku nzuri kwetu kama timu jambo ambalo tunaamini litakuwa
ni nguzo kwetu kwani kama unavyomjua Maximo ni mtu wa watu lakini ni kocha
mwenye misimamo ya kutaka kazi yake ifanyike kwa ufanisi mkubwa,” alisema mmoja
wa maafisa ndani ya dawati la ufundi la Yanga.
Alhamisi wiki hii wakati anazungumza na Wandishi wa Habari, Maximo aliweka
vibaombele vyake ambavyo anaamini vinaweza kuivusha Yanga hapo ilipo na kwenda
mbele zaidi huku suala la kukuza na kuendeleza vipaji, nidhamu ndani na nje ya uwanja ni miongoni mwa mambo aliyoyatilia mkazo.
“Mipango ni mingi lakini kuna mambo ya kuyashughulikia kwa wakati huu,
mopja wapo ni suala la kuendeleza vipaji vipya ambavyo naamini vinaweza
kusaidia katika timu ya Yanga na Tanzania kwa ujumla, hivyo msaidizi wangu
Leonadro Neiva atakuwa na kazi ya kushughulikia soka la vijana,” alisema Maximo
raia ambaye kabla ya kutua Yanga alikuwa akiifundisha timu ya Associacao Atletica
Francana ya jijini Sao Paulo nchini Brazil.
Dawati la unfindi la Yanga hivi sasa litakuwa na makocha watano ambao ni
yeye Maximo mwenyewe kama Kocha mkuu, pamoja na wasaidizi wake watatu ambao ni Leonadro
Neiva kocha msaidizi, Juma Pondamali Kocha wa makipa pamoja na Meneja Hafidh
Saleh huku Kocha msaidizi mzawa akitarajiwa kujulikana baadaye.
Muungo kama huu ndiyo unaotumika kwenye nchi za Ulaya ambazo zimepiga
hatua katika maendeleo ya mpira tofauti na Tanzania ambapo mfumo huu
unaoneakana kuwa ni mpya.
Miongoni mwa mipango ambayo imeanza kushughulikiwa ni suala la usajili
baada ya Maximo kumsajili kiungo raia wa Brazil Andrey Coutinho, ambaye anakuwa
mchezaji wa tatu kutoka nje ya Afrika kusajiliwa na Yanga tangu kuanzishwa
kwake mwaka 1934.
Yanga inalazimika kufanya usajili huo kutokana na kuwepo kwa pango la
wachezaji wawili tegemeo ambao ni kiungo Frank Domayo na shambuliji raia wa Burundi,
Didier Kavumbagu ambao wote waiwli wametimkia Azam FC hivyo ujio wa Countinho
ni moja ya dawa ya kuhakikisha kikosi chake kinakuwa bora.
Hii si mara ya kwanza kwa Yanga kusajili wachezaji kutoka nje ya Afrika
ambapo kwakwani kwa mara ya kwanza, ilimsajili kipa kutoka nchini Serbia Obren Cirkovic katik
usajili wa mwaka 2008.
Kutokana na ubora wake, kipa huyo aliweza kuwa kipa namba moja ndani ya
kikosi cha Yanga ingawa alikuwa akibadilisha na kipa Juma Kaseja katika baadhi
ya mechi huku timu hiyo ikiwa chini ya Kocha raia wa Serbia Dusan Kodic.
Kadhalika katika msimu wa mwaka 2010,
Yanga iliandika historia nyingine baada ya kumsajili kipa kinda kutoka
Serbia, Ivan Knezevic ambaye alidumu kwa misimu miwili kisha kutimkia katika
klabu ya FK Novi Sad ya Serbia.
No comments:
Post a Comment