Marcio Maximo, Kocha wa Yanga
KLABU ya Yanga, imesema kuwa haijapata
ongezeko la dau la kumnunua nyota wao, Mrisho Ngassa kutoka klabu ya Free State
Stars ya Afrika Kusini.
Baada ya kufuzu katika majaribio
hayo, imeelezwa kuwa klabu hiyo ya Afrika Kusini ilituma ofa kwenda Yanga
ambayo ni Doa za kimarekani 80,000 zaidi ya milioni 134 fedha za Kitanzania
ingawa ofa hiyo ilikataliwa kwani Yanga walikuwa kihitaji Dola 150,000, zaidi
ya milioni 250.
Hata hivyo dira ya ulimwengu ilimtafuta
Mwenyekiti wa mashindano wa Yanga ambaye pia mara kadhaa amekuwa akishughulikia
usajili, Seif Ahamed ‘Magari’ alikana kuwa Yanga ilitaka dao hilo la Dola
150,000 ingawa hakutaja kiasi gani kilichopendekezwa.
“Mimi ninafahamu kwamba ofa
kutoka Afrika Kusini ilifika mezani kwetu lakini fedha zilinazoelezwa si za
kweli ila kuna makubaliano ambayo yapo baina ya klabu zote mbili yaani Yanga
pamoja na Free State Stars, ingawa kwa
maelezo zaidi zungumza na Katibu Beno Njovu au Msemaji Baraka Kizuguto,”
alisema Magari ambaye amerejea hivi karibuni akitokea Brazil kuangalia michuano
ya Kombe la dunia.
DIMBA lilimtafuta, Kizuguto
alisema alisema suala la kuongezwa dau hajaipata yeye kama msemaji na kwamba
sujala la biashara ya kumuuza Ngassa katika klabu ya Free State linafanywa na
pande mbili ingawa hakuweza kufafanua zaidi.
“Ninachokifahamu ni kwamba Yanga
ilimruhusu Ngassa kwenda Afrika Kusini kufanya majaribio pamoja na kambi ya
timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliyopo nchini Bostwana.
Katika hatua nyingine, Kocha wa Free State ya Afika Kusini, Mbelgiji, Tom Saintfiet
amemtabiria mambo makubwa Mrisho Ngassa
ikiwemo kucheza soka barani Ulaya kama akifanikiwa kujiunga na klabu
hiyo.
“Kwanza Free State wenyewe hatukaa
naye muda mrefu ila soko la kwenda Ulaya hapa ni kubwa ikilinganisha na maeneo
mengine ya Afrika kwa hiyo kama akifanikiwa kucheza katika kikosi chetu ni wazi
kuwa milango ya ulaya ipo wazi kulingana na falsafa za klabu hii,” alisema
Saintfiet, Kocha wa zamani wa Yanga na timu za taifa za Ethiopia na Malawi.
Ngassa yupo Afrika Kusini kwa
ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa katika klabu hiyo ya Free
State Stars inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet na
tayari imeelezwa kuwa amefuzu.
SALMA JUMA NA SAADA AKIDA wa DIMBA
No comments:
Post a Comment