TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inatarajiwa kucheza
mechi yua kirafiki dhidi ya Lesotho, Julai 5 mwaka huu ikiwa ni siku moja kabla
ya kurejea nchini Julai 6. Stars ipo Gaborone, Botswana ilikoweka kambi ya wiki mbili
kujiandaa na mechi ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika (AFCON 2015) zitakazofanyika nchini Morocco.
Akizungumza na www.dirayaulimwengu.com, Meneja wa kikosi hicho Boniface Clement,
kutoka Botswana , alisema kuwa Kocha Martinus Ignatius ‘Mart’ Nooij ameamua
kucheza mechi hiyo ambapo muhimu kwa ajili ya kukiweka kikosi chake sawa.
“Tutacheza mechi ya kirafiki na Lesotho ikiwa ni mahitaji ya
kocha kabla kurejea nyumbani kwa ajili ya kucheza na Msumbiji, Julai 20 mwaka
huu,” alisema Clement.
Katika hatua nyingine, Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Boniface Wambura, alisema kwamba kikosi hicho kilitarajiwa kucheza mechi ya
kirafiki ya kijipima nguvu dhidi ya wenyeji Botswana leo ambao matokeo yaliyopatikana hivi karibuni ni kwamba imelala kwa mabao 4-2.
Stars ipo kwenye maandalizi makali ya kuhakikisha kwamba
inapata ushindi dhidi ya Msumbuji ambayo haina rekodi nzuri kwenye mechi za
mashindano mara inapokuntana na Mambaz.
Katika hatakati za kutafuta kucheza fainali za Afrika mwaka
2008, Stars chini ya Kocha Marcio Maximo ilikwama baada ya kukubali kufungwa
bao 1-0 na Msumbiji kwenye Uwanja wa Taifa, bao lililofungwa kwa kichwa na
mshambuliaji hatari, Ticotico.
NA ZAINAB IDDY
No comments:
Post a Comment