Samaki aliye na urefu wa mita tatu aliyekuwa maarufu katika mto Amazon amevuliwa hadi ameangamia.
Watafiti wamedhihirisha kuwa samaki huyo mkubwa hapatikani tena katika maeneo aliyokuwa maarufu.Imebainika sasa kuwa samaki wa Arapaima alipatikana katika maeneo 8 kati ya 41 zilizofanyiwa utafiti, na idadi ya samaki huyo ilikuwa ndogo sana kulikoilivyokuwa inatarajiwa.
Wavuvi walipewa mafunzo jinsi ya kuhesabu samaki hao ili kufanikisha utafiti huo mkubwa.
Watafiti walikata kauli kuwa athari za uvuvi kwa samaki wa kitropiki zilikuwa mbaya zaidi ya ilivyoaminika hapo awali.
Matokeo ya utafitihuo yaliripotiwa kwa shirika la uhifadhi wa mazingira yanayozalisha viumbe vya majini ''Aquatic Conservation: Freshwater and Marine Ecosystems''.
Arapaima huweza kuwa na uzani wa kilo 181 na ni mojawapo ya samaki wakubwa zaidi wanoishi katika maji yasiyo na chumvi.
Samaki hao hupumua hewa sawa na binadamu, hivyo basi huibuka kutoka majini kupumua kila baada ya dakika kati ya 10-15 hivyo basi huwa ni rahisi kuwakamata.
Ukubwa wa Arapaima huvutia wavuvi kuwawinda na aghalabu huwanasa kwa kutumia chusa au nyavu za uvuvi.
Karne moja iliyopita, idadi ya Arapaima ilikuwa kubwa katika mto wa Amazon, lakini watafiti wanasema kuvua kupita kiasi kumesababisha idadi hiyo kupungua kwa kiwango kikubwa sana.
Hapo awali, utafiti nadharia ulitabiri kuwa uvuvi hauwezi kuangamiza aina fulani ya samaki majini kwani wavuvi huenda kuvua maeneo tofauti idadi ya samaki inapopungua katika eneo moja.
Wanasayansi, wakiongozwa na Leandro Castello, kutoka Virginia Marekani, walitaka kufahamu afya ya samaki wa Arapaima walioko eneo la chini la Amazon.
Aidha walitaka kugundua iwapo shughuli za uvuvi ziliunga mkono au kupinga utabiri wa nadharia tofauti.
Kuna nadharia zinazopendekeza kuwa samaki wakubwa, walio ghali, na ambao ni rahisi kukamatwa huweza kuvuliwa na kuisha majini, huku nadharia zingine zikipinga msimamo huo.
Watafiti hao walihoji wavuvi 182, walioaminika kuwa magwiji na wenzao, katika jamiii 81, zinazoishi katika eneo la kilomita 1,040, la Amazon.
Shughuli hiyo ilijumuishwa hesabu ya Kulifanywa ya samaki katika jamii 41 kati ya jamii zilizohojiwa.
Wavuvi nane walifunzwa kuhesabu idadi ya Arapaima pindi tu walipotokea majini.
Matokeo ya hesabu hiyo ni kuwa idadi ya Arapaima ilikuwa imepunguka katika asilimia 57% ya eneo la utafiti, Arapaima hawakuwepo katika asilimia 19% ya eneo hilo, na walivuliwa kupita kiasi katika asilimia 17% ya eneo hla utafiti, huku asilimia 5% tu wakifanya uvuvi unaokubalika.
Kwa 2% ya jamii zilizofanyiwa utafiti, samaki hao hawakuvuliwa.
Chanzo cha bbc.swahili