KIONGOZI wa kundi chipukizi la muziki wa dansi
nchini, Yamoto Band, Dogo Aslay, amefunguka kuwa ushiriki wao kwenye tamasha la
'Siku ya Msanii' umeijengea heshima bendi hiyo.
Aslay ameliambia DIMBA Jumatano kwamba, tamasha hilo
lilikuwa na sura ya kitaifa hivyo kupata kwao nafasi ya kutumbuiza kutawasaidia
kuongeza mashabiki na kuheshimika kama ilivyo kwa bendi kongwe za muziki wa
dansi nchini.
"Kwetu tunawapigia saluti waandaji wa siku ya
msanii kutuchaguza kuwa watumbuizaji kwani Tanzania kuna bendi nyingi lakini
tukawa pekee kupata nafasi hiyo.
Katika tamasha hilo wasanii Edward Said Tingatinga
alitunukiwa tuzo ya Msanii aliyejitolea maisha yake yote katika maendeleo ya
sanaa (Lifetime achievement award) na Josephat Kanuti kutoka Morogoro, ambaye
alitunukiwa tuzo ya msanii aliyetoa mchango mkubwa katika jamii kupitia sanaa
(Humanitarian award).
Siku ya Msanii Tanzania, iliandaliwa na kampuni ya
Haak Neel Production na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kudhaminiwa na
Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Bingwa, Dimba,
Rai, Mtanzania na The African, Azam Media, Hugo Domingo, EFM, Mfuko wa Pensheni
wa PSPF, Channel Ten na Magic FM.
No comments:
Post a Comment