NA SAADA SALIM
KAMATI ya Usajili ya Klabu ya Simba imetenga Sh
milioni 170 kwa ajili ya kumnasa winga machachari wa Yanga, Simon Msuva,
ili aisaidie timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara msimu ujao.
Taarifa zisizo na shaka zilizolifikia DIMBA
Jumatano kutoka kwa kigogo mmoja wa Kamati hiyo zinaeleza kuwa tayari
wameshatenga donge hilo kwa ajili ya kumnasa Msuva, ambaye amekuwa na
msimu mzuri ndani ya Yanga kutokana na kuwa mwiba mkali wa kucheka na
nyavu.
"Suala la Msuva kuja Simba halina ubishi wowote, kwani Kamati
inaendelea na harakati za kumnasa winga huyo kwa ajili ya msimu ujao,"
alisema kigogo huyo na kuongeza: "Dau hilo tulilomtengea tuna uhakika
kabisa hawezi kulikataa".
Kwa nyakati tofauti Mwenyekiti wa Kamati
hiyo, Kepteni Zacharia Hanspope, amekiri uwepo wa mpango wa kuipa pigo
Yanga kwa kumchukua Msuva kwa madai kuwa kiwango chake ni kizuri na pia
hata yeye mwenyewe anaipenda Simba, hivyo hawana budi kumrejesha
nyumbani.
No comments:
Post a Comment