Saturday, May 2, 2015

Maximo apata dili Brazil


NA MWANDISHI WETU
KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania na Yanga ya Dar es Salaam, Marcio Maximo amepada dili jipya baada ya kupewa mkataba wa miaka mitatu wa kuinoa timu  ya Prudentópolis ya nchini Brazil.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini Brazil ni kwamba Maximo amepewa jukumu hilo ili kuiweka sawa timu hiyo ambayo ilianzishwa Novemba Mosi mwaka 2007.
Rais wa Prudentopolis, Valdir Luiz Cagnini amekaririwa akisema kuwa wameamua kumchukua Maximo kutokana na uzoefu wake hivyo anaamini atakuwa msaada katika kikosi chao ambacho kinatafuta nafasi ya kuelekea daraja la kwanza msimu ujao.
“Tunaelewa timu yetu bado ni changa lakini tupo kwenye njia ya kutafuta mabafanikio ya kuwa miongoni mwa timu bora katika ligi ya Brazil  lakini kwa kuanzia msimu ujao kama tukipata nafasi ya kupanda daraja.
“Hivyo naamini wazi kuwa sasa tumepata kocha sahihi atakayeweza kutusaidia kupanda na kufanikiwa kama zilivyo nchi nyingine kutokana  na historia ya Maximo katika kazi yake akiwa ndani na nje ya Brazil,” alisema Cagnini.
Prudentopolis ipo daraja la pili kutoka jimbo la Parana lililopo Kusini mwa Brazil ambapo inatumia Uwanja wa Newton Agibert wenye uwezo wa kubeba mashabiki 3,500, ukiwa ni moja ya viwanja vidogo zaidi nchini Brazil.
Kocha Maximo aliliwa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars tangu mwaka 2006 hadi 2010 na baadaye kuzifundisha timu mbalimbali ambazo ni Democrata-GV na Francana zote za Brazil na baadaye kujiunga na kikosi cha Yanga Juni 28 mwaka 2014 na kwenye msimu wa ligi alifukuzwa.

No comments:

Post a Comment