Tuesday, December 29, 2015

Hiki ndicho akilichokisema Prof: Jay

Mbunge wa jimbo la Mikumi mkoani Morogoro, Joseph Haule amesema kuwa leo ametimiza miaka 40 lakini akiwa na furaha kubwa kwani ndiyo amekabidhiwa rasmi ofisi ya Mbunge jimbo la Mikumi.

Katika taarifa yake yenye mameno machache kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Facebook alisema kwamba:-

Asante sana Mungu leo nimetimiza miaka 40 tangu Nimezaliwa .... I dedicate this birthday kwa watu wangu wote wa MIKUMI na leo ndio tumeifungua rasmi ofisi ya MBUNGE ya MIKUMI baada ya kukabidhiwa Funguo na kuifanyia Usafi kwa pamoja tayari kwa kusikiliza changamoto za wana mikumi, Ushauri na maoni ya jinsi gani tunashirikiana pamoja na wana Mikumi kuweza kuleta mabadiliko na maendeleo ya MIKUMI YETU... EEE MWENYEZI MUNGU TUSAIDIE!!!.


Akifanya usafi ofisini kwake


 Akila kiapo kuwa mbunge wa Jimbo la Mikumi

 

 Akiwa anaingia Bungeni kwa mara ya kwanza


 Akiwa kwenye kikao cha madiwani

Akitekeleza shughuli za maendeleo kwenye usimamizi wa barabara jimbo la Mikumi

Monday, December 28, 2015

Yanga wamfukuza Niyonzima

Uongozi wa Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, umemfukuza rasmi kiungo wake wa kimataifa raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu.

Taarifa ya uongozi wa Yanga imesema kwamba wameamua kuchukua maamuzi hayo kutokana na mwenemdo wa nyota huyo katika utendaji wake wa kazi lakini pia kwa sababu alivunja kipengere kwenye mkataba wake na Yanga.

TAARIFA KAMILI HII HAPA:


 

Saturday, December 26, 2015

Waporaji wauawa Mbagala Kuu


VIJANA wa wawili katika eneo la Mbagala Mkuu wameuawa na wananchi wenye hasira badaa ya kupora beki la mwanamke mmoja mkazi wa Mbagala Kuu.
Tukio hilo lilitokea katika mtaa wa njia ya jeshini lafajiri ya leo ambapo baada ya kupora vijana hao waliokuwa watatu wakiwa na mapanga, bisibisi na vyembe walikimbia hadi mtaa wa makonde ambapo ndipo walipokamatwa na kisha kushambuliw ana wananchi wenye hasira wakiwa na silaha za jadi. 
katika tukio hilo mmoja ya vijana hao aliweza kukimbia na kufanikiwa kupona lakini mmoja alikimbilia kwenye moja ya choo kilichokuwa kwenye moja ya nyumba za mtaa huo ambapo wananchi hao walimfuata na kutoa kisha kupiga ambapo alimkata kata kisha kumuunganisha na mwenzake ambao waliwekwa kwenye eneo la wazi kisha kuchomwa moto.
Hata hivyo walikuonekana baadhi ya kina mama wakilia na wengine wakilaani tukio la kuuawa kwa vijana hao ambao hadi sasa bado hawajaweza kutambulika majina yao.
Katika siku za hivi karibuni eneo la Mbagala Kuu wameibuka vijana ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya uporaji na uharibifu wa mali.
Desemba 24 mwaka huu mwanamke mmoja alipora kisha kubakwa na vijana ambao hawakufahamika mara moja wakati mwanamke huyo akitokea kazini majira ya saa 3:00 usiku.
Mbali na tukio hilo kumekuwepo na matukio ya kuvamiwa na kuporwa mali watu mbalimbali wakiwa kwenye mageti ya nyumba zao wakiwa wanasubiri kufunguliwa jambo lililozusha hasira kutoka kwa wananchi mbalimbali wa kato hiyo.

Thursday, December 24, 2015

Yanga yapeleka majina 24 CAF




NA SAADA SALIM
KOCHA Mkuu wa Yanga Mholanzi, Hans Pluijm, ana hasira za msimu uliopita kushindwa kuifikisha timu hiyo pazuri kwenye michuano ya kimataifa lakini safari hii ameapa lazima kieleweke.
Unajua kwanini? Mholanzi huyo safari hii amepeleka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), majina ya silaha zake 24 huku 10 zikiwa za kimataifa tayari kwa kufanya makubwa mapema Februari mwakani kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika majina hayo 24 ukiwaacha, Thaban Kamusoko, Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima, Issoufou Boubacar Garba, Vicent Bossou na Mbuyu Twite, Pluijm ameamua kuleta majembe mengine mawili ya kimataifa ingawa tayari inaye mchezaji mmoja Mnyarwanda, Jerome Sina, anayefanyiwa majaribio.
DIMBA Jumatano limethibitishiwa kwamba Yanga itawaleta straika, Spencer Sautu kutoka Ashanti Gold ya Ghana, ambaye ataungana na beki shupavu aitwae Kabongo kutoka Congo (DRC).
Wawili hao wanakuja wakati wowote nchini kuanzia sasa kufanya majaribio ingawa inaelezwa kwamba kocha Hans anavifahamu vyema viwango vyao vya soka.
Chanzo cha habari cha uhakika kimelieleza gazeti hili kuwa ujio wa wawili hao utafanya timu hiyo iwe na wachezaji 10 wa kimataifa ili kukifanya kikosi chao kiweze kuhimili vishindo vya michuano hiyo mikubwa zaidi barani Afrika na yenye utajiri mkubwa inayoandaliwa na CAF.
Aidha, chanzo hicho kilieleza kuwa Yanga bado inaendelea kumfanyia majaribio kiungo wa Rayon Sport, Jerome Sina, ingawa usajili wake utasubiri kwanza ili kulinganishwa kiwango na Sautu.
Jerome mwenye miaka 26 raia wa Congo (DRC) amemvutia Pluijm na inaelezwa iwapo atafuzu majaribio atasajiliwa mwishoni mwa msimu kwa ajili ya kuibeba Yanga.
"Sasa hivi hatutaki masihara kwani tunahitaji kufika mbali zaidi, ukiangalia msimu uliopita hatukufikia malengo yetu kwa vile tulitolewa mapema ndiyo maana usajili wa wachezaji wa kigeni unafanyika kwa umakini mkubwa tukiamini watasaidiana vyema na wazawa ili mwakani tuweze kuvunja rekodi yetu," alisema mtoa habari.
Alisema tayari benchi la ufundi la timu hiyo limependekeza kupeleka idadi ya majina 24 kwa ajili ya michuano hiyo ya kimataifa ambapo wachezaji hao wawili wanaotarajia kutua hapa nchini wataungana na Sina kwa ajili ya majaribio na baadaye kusaini.
Katika hatua nyingine, Yanga imebadilisha mipango yake ya kwenda kujifua nchini Ghana kwa ajili ya kujiandaa na michuano hiyo na badala yake watabaki hapa nchini na kuzialika timu za nje ili kucheza nazo mechi za kujipima.
Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm, ameliambia DIMBA Jumatano kuwa wana mpango wa kuzialika timu tatu za kimataifa ambazo ni Ashanti Gold ya Ghana pamoja na Gor Mahia na KCB zote za Kenya.
"Mpango wetu wa kwenda nje ya nchi umekufa kutokana na ratiba kuingiliana, lakini tumezialika timu nne ambapo mbili za KCB na Gor Mahia tayari zimethibitisha huku Ashanti ikiwa bado," alisema kocha huyo.