Monday, July 28, 2014

10 wakamatwa na silaha Dar

http://htmlimg1.scribdassets.com/82eocnbjy83ypdpz/images/1-290c089e1f.jpg 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI JESHI LA POLISI TANZANIA PRESS RELEASE 28/07/2014

MAJAMBAZI 10 HATARI WAKAMATWA NA SILAHA/BUNDUKI NANE MMOJA MWANAMKE ANAYEJUA KUTUMIA SMG.



                                      Kamanda Kova
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limefanikiwa kukamata mtandao hatari wa majambazi wapatao kumi (10) mmoja wao akiwa ni mwanamke anayeshiriki kikamilifu wakati wa matukio ya ujambazi. Majambazi hao wamekamatwa katika msako mkali unaoendelea jijini Dar es Salaam katika harakati za kuhakikisha kwamba maisha na mali za wakazi wa Dar es Salaam vinalindwa kikamilifu.
Katika msako huo watuhumiwa walipekuliwa katika miili, makazi, na maficho yao na wakakamatwa na  jumla ya silaha 8 kama ifuatavyo.
1. SMG NO. 13975 ikiwa na risasi 11 na magazine 2
2. SMG 1 haikuwa na magazine na namba hazisomeki.
3. BASTOLA 1 aina ya LUGER yenye namba 5533K
4. BASTOLA 1 aina ya BROWNING yenye namba TZACR83494 S/No.7670 Na risasi 6 ndani ya magazine.
5. S/GUN PUMP ACTION na risasi 55
6. MARCK IV iliyokatwa mtutu na kitako yenye magazine 1 na risasi 4
7. BASTOLA 1 yenye namba A963858 browning ambayo ina risasi 1
8. SMG 1 ambayo iko kwa mtaalam wa uchunguzi wa silaha (Balistic)
9. SHOT GUN TZ CAR 86192 ilitelekezwa baada ya msako.

Majina ya watuhumiwa ni ifuatavyo:-
1. MAULIDI S/O SEIF MBWATE miaka 23, mfanyabishara, mkazi wa Mbagala Charambe.
2. FOIBE D/O YOHANES VICENT miaka 30, hana kazi, mkazi wa Mbagara Kibondemaji.
3. VICENT S/O OGOLA KADOGOO miaka 30, mkazi wa Mbagara Kibondemaji
4. SAID S/O FADHIL MLISI miaka 29, dereva wa Bodaboda, Mkazi wa Gongolamboto
5. HEMEDI S/O AWADHI ZAGA miaka 22, dereva wa Bodaboda, mkazi wa Gongolamboto
6. MOHAMED S/O IBRAHIM SAID miaka 31, Fundi welder mkazi wa Kigogo.
7. LUCY MWAFONGO. Miaka 41, mama lishe mkazi wa Vingunguti Ukonga
8. RAJABU S/O BAHATI RAMADHANI, miaka 22, Mkazi wa Kariakoo
9. DEUS JOSIA CHILALA miaka 30, Mgonga Kokoto Kunduchi , mkazi wa Yombo Kilakala.
10. MARIETHA D/O MUSA miaka 18, mkazi wa Yombo Kilalakala Mwanamke pekee katika kundi hilo anayejulikana kwa jina la FOIBE D/O YOHANES VICENT ameshiriki katika matukio ya uporaji wa kutumia silaha, mauaji, n.k. na yeye mwenyewe alikuwa akitumia bunduki aina ya SMG.
Katika baadhi ya matukio wananchi walioshuhudia matukio haya wamekuwa wakitoa taarifa kwamba alikuwepo mwanamke aliyekuwa akifyatua risasi na hatimaye polisi walifanikiwa kumkamata akiwa na wenzake katika kundi hilo.
Licha ya kukamatwa kwa mtandao huu hatari Jeshi la Polisi linaendelea na misako ya mitandao mingine ya ujambazi kwa madhumuni yaliyotajwa hapo juu. Hivyo tunawashukuru wananchi kwa namna walivyoendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutokomeza uhalifu.
Majambazi hao watafikishwa mahakamani baada ya Mwanasheria wa Serikali kupekua majalada yao ya kesi mbali mbali.

MITAMBO NA VING’ORA KATIKA TAWI LA STANBIC BANK KARIAKOO
VYAWAKIMBIZA/KUWAKURUPUSHA MAJAMBAZI KABLA YA KUKAMILISHA DHAMIRA YA KUPORA FEDHA ZA BANK Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limeanzisha msako mkali wa kuwatafuta majambazi watano ambao jana tarehe 27/7/2014 saa 8.00 mchana walifika katika benki ya Stanbic Tawi la Kariakoo lililoko mtaa wa Swahili.
Watatu kati yao waliingia ndani ya benki hiyo wakiwa na mifuko mikubwa wakijifanya ni wateja waliopeleka fedha nyingi katika benki hiyo. Watu hao watatu walipoingia ndani walianza kulazimisha kuvuka wigo wa wateja wa kawaida na kutaka kuingia kwa nguvu kwenda kupora fedha.

Stanbic Bank ina mitambo ya aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na ving’ora vya tahadhari. Ving’ora hivyo vilianza kulia kwa sauti kubwa nje na ndani ya benk hiyo hali iliyowatia kiwewe wahalifu hao.
Waliamua kurudi nje kwa kasi ambapo kulikuwa na gari aina ya Noah na pikipiki moja ambazo hazikusomeka namba kwa haraka na wakatoweka baada ya kufyatua risasi hewani na kuwatisha watu waliokuwa nje na ndani ya Benk.
Baada ya kuondoka majambazi hao iligundulika kwamba mmojawao alichota kwa mkono kiasi cha fedha ambazo mteja alizileta kwa madhumuni ya kuziweka katika Tawi hilo.
Baada ya kutoroka majambazi hao waliterekeza mifuko mikubwa ambayo walitegemea kubebea fedha watakazopora katika benk hiyo ambayo imehifadhiwa kama kielelezo na ndani ya mifuko hiyo waliweka kokoto na uchafu mwingine kwa madhumuni ya kuwadanganya walinzi na watumishi wa benk kwamba walikuwa wamebeba fedha za kuweka benki.
Kutokana na tukio hili tunahimiza benki zote kuchukua tahadhari za kiusalama ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba wanaingia mkataba wa kulindwa na Jeshi la Polisi, kuweka vifaa mbali mbali vya ulinzi vikiwemo ving’ora (alarms), CCTV Camera na mashine za kugundua (metal detectors) mtu anapoingia na silaha au kitu kingine cha hatari kama visu, mitarimbo n.k.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TAHADHARI YA KIUSALAMA KUELEKEA SIKUKUU YA IDD EL HAJI 2014.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeweka mikakati ya mpango kazi kama ifuatavyo:-
Limepanga kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Kampuni binafsi za ulinzi, Vikosi vya uokoaji wakati wa majanga, na vikundi vya Ulinzi Shirikishi ili kuhakikisha kuna udhibiti wa matukio ya uhalifu au fujo zinazoweza kujitokeza.
Tumejipanga kutumia Kikosi cha FFU kikijumuisha askari na magari ya washawasha, Askari wa Mbwa na Farasi. Kikosi cha Polisi Wanamaji nacho kitakuwepo. Pia Vikosi vya Kuzuia Dawa za Kulevya, askari wa kawaida (GD), askari wa Usalama Barabarani, na askari Makachero.
Wote hawa wamepewa maagizo maalum ya kuchukua hatua kabla matukio ya uhalifu hayajajitokeza na sio kungoja tukio lifanyike.
Kwa mantiki hiyo, dalili zozote za uvunjifu wa amani litashughulikiwa pasi na ajizi. Zitakuwepo doria za Miguu, doria za pikipiki na doria za miguu katika barabara zote muhimu.

Wananchi wanashauriwa kusherehekiea siku ya Idd El Haji katika ngazi ya familia au kukusanyika katika mitaa kwa amani wakisherehekea.


1. RPC ILALA: Mary Nzuki  – SACP 0754 009 980 / 0754 339 558 2.

2. RPC TEMEKE: Kihenya wa Kihenya – SACP 0715 009 979/ 0754 397 454 3.

3. RPC K’NDONI: Camillius Wambura – ACP 0715 009 976 / 0684 111 111.

“NAWATAKIA NYOTE HERI YA IDD EL FITR
2014”.

S.H. KOVA

KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM.

maendeleo ya Bahati Bakuku baada ya kupata ajali Dodoma




(Picha mbalimbali za ajali ya Bukuku na nyingine zikimuonyesha akiwa Hospitali kwa ajili ya matibabu)
Usiku , muimbaji nyota wa nyimbo za injili, Bahati Bukuku pamoja na wasaidizi wake, walipata ajali akiwa njiani kuelea Kahama kwenye huduma. paparazi ilikuripoti taarifa za awali, na hapa tunakuletea picha kamili na taarifa rasmi ya jeshi la polisi mkoani Dodoma.

Juhudi za kumhamishia Bahati Bukuku kuelekea Muhimbili kama ilivyopangwa awali zimeshindikana, kutokana na kushindwa kugeuka wala kuinuka akiwa amelazwa. Tayari ndugu na marafiki walishafika kutoka Dar es


Salaam, na watu kadhaa wa Dodoma na viunga vyake walipita kuwajulia hali na kuwafariji.

Taarifa ya Jeshi la Polisi, Dodoma.
Gari lenye namba IT 7945 Toyota Nadia likiendeshwa na EDSON MWAKABUNGU (31) mkazi wa Tabata Dar es Salaam liliacha njia na kugonga gema na kusababisha majeraha kwa watu watatu baada ya kugongwa na gari jingine linalosadikiwa kuwa Fuso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime SACP amesema ajali hiyo imetokea tarehe 26.07.2014 saa tisa alfajiri katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma eneo la Ranch ya NARCO Wilaya ya Kongwa.

Waliojeruhiwa ni EDSON MWAKABUNGU ambae analalamika maumivu sehemu za vidole vya miguu yote, BAHATI BUKUKU (40) ambae ni mwimbaji wa nyimbo za injili na mkazi wa Tabata – Dar es Salaam ambaye analalamika maumivu sehemu mbalimbali za mwili wake.

Mwingine ni FRANK CHRISTOPHER (20) mwimbaji pia wa nyimbo za injili mkazi wa Tabata Dar es Salaam ambapo kapata michubuko usoni na mkono wa kulia.

Wote wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri ambapo Kamanda Misime amesema walikuwa wanatokea Dar es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo, BAHATI  BUKUKU na FRANK  CHRISTOPHER walikuwa wanakwenda Kahama kwenye tamasha la Injili.

Uchunguzi wa ajali hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.

Saturday, July 26, 2014

Hii ndiyo Afghanistan kabla ya kuutawala wa Taleban ndani ya nchi hiyo.

Kabla ya kuingia kwa utawala wa taleban, taifa la Afghanistani lilikuwa ni miongoni mwa mataifa yenye ustawi mzuri na lisilokuwa na ubaguzi wala mgawanyiko wowote baina ya watu ikiwemo wanawake na wanaume walikuwa wakisafiri pamoja, wanawake halikuwa wanaruhusiwa kutembea vichwa wazi, pia watoto wa kike walikuwa wa kipata elimu sawa kama ilivyo kwa wanaume. 
Hizi ni baadhi ya picha kutoka maktaba mbalimbali duniani zikionyesha taifa hilo kabla ya kuingia kwa Taleban iliyokuwa chini ya Mullar Omar.
 Mtaani
 Kizuizi cha gari lililokiuka sheria
 Usafiri wa umma kwa watu wote
 Mavazi na tamaduni ilikuwa ipo hivi!
 Watoto wa kike walikuwa wakipata elimu sawa na wale wa kiume!
 Hiki ni kituo za kujaza gesi.
 Hili daraja lililojengwa na Warusi







 Darasa kwa shule za vijijini
Shule za mjini
 Mitaa maarufu na moja ya msikiti maarufu jijini Kabul
 Ukarabati wa mitaa ulikuwa ni sehemu ya utamaduni wa watu wa taifa hilo, kimsingi walikuwa wakiishi kijamaa lakini kwa upndo mkubwa miongoni mwao na wageni pia.

 Paredi ya askari wa Afghanistan
Darasa
Shule za awali
  Chuo kikuu cha Kabul
 Sokoni napo hali ilikuwa iko hivi
 Utengenzaji wa keki

 Mapumziko baada ya shughuli za kutwa nzima
 Kumbukukumbu hii ya kubudha ilibomolewa na Taliban

Hood yapata ajali likitokea Mbeya




Muda mchache baada ajali kutokea.
 Askari wa usalama wa barabarani wakiwa wamefika eneo la tukio  na baadhi ya Mashuhuda wakishuhudia ajali hiyo




 Basi la Hood limepata ajali asubuhi hii likitoka Mbeya haijafahamika mara moja lilikuwa linaelekea wapi na haijafahamika kama kuna watu waliojeruhiwa, endelea kufutilia hapa kupata taarifa kamili hii ni taarifa ya awali.

Bukuku apata ajali Dodoma


Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba, mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili hapa nchini, Bahati Bukuku amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali mbaya katika eneo la Kongwa, mkoani Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, mwimbaji huyo alipata majeraha makubwa sehemu mbalimbali mwilini na kwamba chanzo cha ajali hiyo kinadhaniwa kuwa ni mwendo kasi.
Chanzo hicho hakijaweza kueleza zaidi kwamba Bukuku alikuwa akielekea ama kutoka mkoani Dodoma na kama ndani ya gari hilo kulikuwamo na abiria wengine.
Pia haikuweza kufahamika mara moja kama mwimbaji huyo alikuwa akiendesha mwenyewe gari hilo, ingawa kilithibishwa ajali hiyo na kwamba Bukuku alijeruhiwa vibaya hasa sehemu ya kiuno.
Endelea kuperuzi blogu hii kwa habari zaidi ya tukio hilo.

Friday, July 25, 2014

MKUU WA SHULE ILIYOONGOZA KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA 6 AHAMA NYUMBA

SHULE ya Igowole, iliyoshika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka huu, inakabiliwa na matatizo mengi, ikiwemo ukosefu wa mabweni, kiasi cha Mkuu wa Shule kulazimika kuhama nyuma kuachia wanafunzi wapate pa kulala.

Mbali na ukosefu wa mabweni ya kuhimili idadi ya wanafunzi, matatizo mengine ya shule hiyo ni ukosefu wa maji, maktaba, vifaa vya kufundishia na kusomea, gari la shule na walimu hasa wa masomo ya Sayansi na Hisabati.

Mkuu wa shule hiyo ya serikali iliyoko katika Kijiji cha Igowole wilayani Mufindi, Andrew Kauta, ameachia nyumba kwa ajili ya sehemu ya wanafunzi wa kike 237 wanaojiunga na kidato cha tano shuleni hapo.

Hata hivyo, shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1988 na kidato cha tano na sita kuanza mwaka 2008, pamoja na matatizo hayo, imeongoza kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita ya mwaka huu, yaliyotangazwa hivi karibuni.

Kati ya wanafunzi 30 waliohitimu Kidato cha Sita mwaka jana, 19 walipata daraja la kwanza, 10 daraja la pili na mmoja ndiye mwenye daraja la tatu.

Kitendo cha kuibuka na matokeo mazuri, licha ya kuwepo changamoto hizo, kimekuna wadau wengi akiwemo Mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola ambaye amesema mafanikio ya shule hiyo yanaonesha jinsi walimu na wanafunzi wake wasivyokatishwa tamaa.

Alisisitiza upo umuhimu mkubwa wa kupewa misaada wanayohitaji ili wafanye vizuri zaidi. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkuu wa Shule alisema tangu kuanzishwa kwa shule hiyo, haijawahi kupokea wanafunzi wengi wa Kidato cha Tano kama ilivyotokea mwaka huu.

“Tangu elimu ya kidato cha tano na sita ianze kutolewa shuleni hapa mwaka 2008, tumekuwa tukipokea wastani wa wanafunzi 30 wa kidato cha tano kila mwaka,” alisema Mkuu huyo.

Alisema mwaka huu, shule hiyo imeletewa wanafunzi wa kike 237 wa Kidato cha Tano, watakaoungana na 30 walioingia kidato cha sita. Shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 900 kidato cha kwanza hadi cha sita.

Hata hivyo, mkuu huyo alisema shule ina bweni moja pekee lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi wasiozidi 86. Alisema bweni hilo lililojengwa tangu shule ilipoanzishwa, miaka 26 iliyopita, haliko katika hali nzuri.

Alisema wanafunzi takribani 30 wa Kidato cha Tano, watajibana katika nyumba hiyo huku wengine 36 wakipelekwa katika bweni hilo pekee. Wanaobaki watahifadhiwa katika madarasa matatu, yanayotumiwa na wanafunzi wa vidato vya chini.

Mwalimu wa Taaluma, Isiaka Chodota alisema kutokana na sehemu ya madarasa kutumika kama mabweni, shule inabakiwa na vyumba 19 vya madarasa.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Evarista Kalalu na Mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola waliahidi kuongeza kasi ya kushughulikia matatizo ya shule hiyo, waliyoieleza kwamba mafanikio yake yameutoa kimasomaso mkoa wa Iringa.

Akizungumzia siri ya mafanikio ya shule hiyo katika matokeo ya Kidato cha Sita, Mkuu wa Shule alisema mwaka 2010 walijiwekea mpango mahususi wa miaka mitano wa kuboresha elimu katika shule hiyo, ikiwa ni pamoja na kusisitiza matumizi ya Kiingereza.

Siri nyingine ya mafanikio ya shule hiyo ni kuipa kipaumbele nidhamu. Kwa mujibu wa mkuu wa shule, kila Ijumaa huhakikisha wanafunzi na walimu wanakumbushwa sheria, kanuni na miiko ya shule.

Chanzo: Habarileo

SERIKALI YAPOKEA MABEHEWA 25 YENYE THAMANI YA SH.BILIONI 4.3 KUTOKA INDIA

 Waziri wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe (kulia), akiangalia moja ya mabehewa kati ya mabehewa 25 mapya ya kubebea kokoto yenye thamani ya sh.bilioni 4.3 aliyoyapokea kutoka Kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industriles Limited ya India Dar es Salaam Leo, kwa ajili ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL). Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Mhandisi Kipalo Kisamfu.
 Waziri wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe (katikati), akifurahia jambo wakati wa kupokea mabehewa hayo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Mhandisi Kipalo Kisamfu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk.Shaaban Mwinjaka.
 Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Mhandisi Kipalo Kisamfu (mwenye tai kushoto),akimuelekeza jambo Waziri Mwakyembe.
 Waziri Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari wakati akipokea mabehewa hayo.
 Wafanyakazi wa  Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) na wa TRL wakishusha toka katika meli moja ya mabehewa hayo.
 Baadhi ya wanahabari waliokuwepo kwenye hafla hiyo.
 Wafanyakazi wa  Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) na wa TRL wakishusha toka katika meli moja ya mabehewa hayo.
 Waziri Mwakyembe akiangalia moja ya mabehewa hayo.
 Baadhi ya mabehewa hayo yakiwa yamepangwa katika njia yake bandarini baada ya kushushwa kutoka katika meli.
 Fundi wa Shirika la Reli Tanzania , Ephrahim Joel akikaza nati ya moja ya mabehewa hayo.
Fundi wa Shirika la Reli Tanzania , Francis Mpangala naye akikaza nati katika moja ya mabehewa hayo. (Imeandaliwa na mtandao wa  habari za jamii.com.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imepokea mabehewa 25 mapya ya kubebea kokoto yenye thamani ya sh.bilioni 4.316 kwa ajili ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kutoka Kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industriles Limited ya India.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kupokea mabehewa hayo Dar es Salaam leo, Waziri wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe alisema mabehewa hayo ni sehemu ya mpango kabambe wa Serikali wa kufufua Kampuni ya Reli Tanzania chini ya mapngo wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa sasa (BRN).
Alisema mpango wa BRN kwa Kampuni ya Reli Tanzania umelenga kuiwezesha kampuni hiyo kiutendaji ili iweze kusafirisha tani milioni 3.0 ifikapo mwaka 2016 kutoka tani 200,000 zilizosafirishwa mwaka 2012 kupitia Reli ya kati.
"Katika harakati za kufikia malengo haya makubwa, Serikali kupitia bajeti zake za mwaka 2012/2013 na 2014, ilitenga fedha kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali iliyolenga kuboresha vitendea kazi vya Kampuni ya Reli Tanzania" alisema Mwakyembe.
Alitaja miradi iliyopangwa ni  pamoja na kujenga upya vichwa vya Treni 8, kununua vinchwa vya treni vipya 13, mabehewa mapya 274 ya kubebea mizigo na mabehewa ya breki.
Mwakyembe alitaja mradi mwingine ni kununua mashine ya kushindilia kokoto, kununua mabehewa 22 mapya ya abiria na kununua mabehewa 25 mapya ya kubebea kokoto ambayo yamepokelewa jana.
Katika hatua hiyo Mwakyembe ametumia fursa ?hiyo  kuipongeza TRL kwa kupokea mabehewa hayo kwa wakati na kuishukuru Kampuni ya Hindusthan Engineering and Industries Limited ya India kwa utengenezaji wa mabehewa hayo kwa muda uliopangwa.
Alisema lengo ni kuiwezesha TRL kufikia malengo ya kusafirisha mizigo tani 3.0 na kutembeza treni za abiria tano kwa wiki ifikapo mwaka 2016.
Picha, habari kwa hisani ya michuzi.com