Tuesday, August 25, 2015

KIM KADASHIAN ni mjamzito

Mwanadada matata Kim Kadashian ametangaza kuwa ni mja mzito wa miezi sita na hii imekuwa ni taarifa ya kwanza kutolewa katika siku za karibuni ambapo mwanadada huyo ambaye ni mke wa mwanamuziki nyota, Kanye West ambao kwa pamoja wamakuwa wakimya juu ya suala la la ndoa.
Pomoja na uja uzito wake huo mwanamama huyo ameshindwa kusema lolote juu ya kama atajifungulia nchini Marekani au nchini Israel kwani taarifa nyingine zimeeleza kuwa kuna uwezekano akaenda kujifungulia nchini Israel.

Islamic States waharibu uridhi wa dunia

Julai mwaka huu, kundi la Islamic Stats lililpo nchini Syria limeharibu historia ya dunia baada ya kuvunja sanamu la Simba wa Al-lat, nje kidogo ya mji wa kihistoria wa Palmyra ambao yapo makumbusho ya Palmyra ambao yapo kwenye ofodha ya uridhi wa dunia. Samamu hilo lilijengwa katika karne ya kwanza baada ya Kristo (1st century BC).







 

Mambo ya mazoezi hayo

Hapa ndiyo mambo ya mazoezi kama yanavyoonekana kwenye picha mbalimbali zilizopigwa chini Uingereza hivi karobuni hii ambapo mwanadada Loyce amejaribu kuonyesha uwezo wake katika kutanua na kunyoosha viungo vyake.









Saturday, August 22, 2015

Yanga watetea tena ngao ya jamii

Yanga ya Dar es Salaam imefanikiwa kuitetea tena ngao yake ya jamii kwa mara ya ushindi wa penalti wa mabao 8-7 katika mechi iliyokuwa ngumu na yenye mvuto wa aina yake.
Pamoja na ushindani huo lakini hakuna timi iliyoweza kupata bao ndani ya dakika 90 kwani kila mtu upande ulikuwa ukishamnbulia kwa kutengeneza mazingira bora ya kupata ushindi ila hilo halikufanikiwa.
waliop[ata na kukosa penalti ni kama ifuatavyo:

Waliopata na kukosa penalti mechi ya Ngao ya Jamii Uwanja wa Taifa

Kelvin Yondani-Yanga (anapata)
Ame Ally -Azam (anakosa)
Mbuyu Twite-Yanga (anapata)
Shomari Kapombe-Azam (anapata)
Kamusoko-Yanga (anapata)
Erasto Nyoni-Azam (anapata)
Godfrey Mwashiuya-Yanga (anapata)
Migi-Azam (anapata)
Coutinho-Yanga (anapata)
Morris-Azam (anapata)
Amis Tambwe-Yanga (anapata)
Serge Wawa-Azam (anakosa)
Deus Kaseke-Yanga (kapata)
Himid Mao -Azam (anapata)
Haruna Niyonzima (anapata)
John Bocco-Azam (anapata)
Nadir Horoub Cannavaro-Yanga (kakosa)
Kipre-Azam (kapata)
 

REKODI YA YANGA NA AZM FC LIGI KUU: 

Machi 19, 2014; 
Yanga SC 1-1 Azam FC
Septemba 22, 2013; 
Azam FC 3-2 Yanga SC
Februari 23, 2013;  
Yanga SC 1-0 Azam FC (Ngao ya Jamii) 
Novemba 4, 2012;  
Azam FC 0-2 Yanga SC
Machi 10, 2012; 
Yanga SC 1-3 Azam FC
Septemba 18, 2011;  
Azam 1-0 Yanga SC
Machi 30, 2011;  
Yanga SC 2-1 Azam FC
Oktoba 24, 2010; 
Azam FC 0-0 Yanga SC
Machi  7, 2010;  
Yanga SC 2-1 Azam FC   
Oktoba 17, 2009; 
Azam FC 1-1 Yanga SC
Aprili 8, 2009;  
Yanga SC 2-3 Azam FC
Oktoba 15, 2008;  
Azam FC 1-3 Yanga SC
Septemba 14, 2014
Yanga SC 3-0 Azam FC (Ngao ya Jamii)
Desemba 28, 2014
Yanga SC 2-2 Azam FC
Mei 6, 2015
Azam FC 2-1 Yanga SC
MABINGWA WA NGAO
2001: Yanga SC  2-1 Simba
2009: Mtibwa Sugar  1-0 Yanga SC
2010: Yanga SC  0-0 Simba (3-1penalti)
2011: Simba SC   2-0 Yanga SC
2012: Simba SC  3-2 Azam FC
2013: Yanga SC 1-0 Azam FC
2014: Yanga SC 3-0 Azam FC
2015: Yanga SC 8-7 Azam FC (penalti)
 

Wednesday, August 19, 2015

Kerr airudisha Simba ya 2003



Kikosi cha Simba cha mwaka 2003, kutoka kushoto waliosimama ni  Emmanuel Gabriel,****,  Muso, Alex, Victor Costa, Suilman Matola, waliochuchumaa kutoka kushoto, Ramadhan Waso, Ulimmboka Mwakingwe, Juma Kaseja, Athuma Machupa na Boinicafe Paswasa.

NA EZEKIEL TENDWA
 UNAIKUMBUKA ile Simba ya mwaka 2003? Ilikuwa timu hatari ambayo ilitingisha bara hili la Afrika hasa baada ya kuwavua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa, Zamaleck ya Misri na kuleta shangwe kwa mashabiki na Watanzania kwa ujumla.
 Kwa sasa mashabiki wa Simba wanayo kila sababu ya kuanza kutabasamu baada ya kikosi hicho kuwa moto wa kuotea mbali ikipikwa vya kutosha na kocha wake mkuu, Dylan Kerr na haitakuwa ajabu zama zile zikarejea tena.
 Simba ile ya 2003 ambayo ilikuwa chini ya kocha kutoka Kenya, James Siang’a, ilisheheni wachezaji hatari kila idara kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili, Evans Aveva ambaye kwa sasa ni Rais wa klabu hiyo.
Uongozi wa Simba kwa sasa chini ya Aveva wameanza kuweka mipango kabambe ya kuhakikisha kikosi chao kinaanza kuonyesha makucha yao wakipania kuibuka mabingwa msimu unaokuja ili kufanikiwa kucheza michuano ya kimataifa. 
Kwa misimu mitatu mfululizo Simba wameshindwa kumaliza moja ya nafasi za juu na sasa wameweka wazi kwamba wataingia katika ligi wakiwa nguvu moja ili kupata kile ambacho wamekikosa kwa muda mrefu.
Katika michezo yake ya kirafiki wameonyesha kandanda la kuvutia wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 katika tamasha la Simba Day dhidi ya SC Villa ya Uganda na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya URA pia ya Uganda michezo yote ikichezwa Uwanja wa Taifa.
 Kamati ya usajili ya Simba chini ya Zacharia Hanspope na msaidizi wake, Kasim Dewji, wamekuwa wakihangaika huku na kule kuhakikisha wanapata wachezaji wazuri watakaokidhi matakwa na benchi la ufundi kitu ambacho kwa kiasi fulani wamefanikiwa.
Simba ya mwaka 2003 ilikuwa chini ya mwenyekiti wake, Ahmed Balozi, Katibu mkuu akiwa Kasim Dewji ambaye kwa sasa ni msaidizi wa Hanspope katika kamati ya usajili, huku Aveva ambaye kwa sasa ni Rais wa klabu hiyo alikuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili.
Kikosi hicho ambacho kiliwatoa mabingwa watetezi wa ligi hiyo ya mabingwa Afrika, Zamalek, kiliundwa na mlinda mlango, Juma Kaseja, Said Sued, Ramadhan Wasso, Boniface Pawasa, Victor Costa, pamoja na Seleman Matola aliyekuwa nahodha ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi.
Wengine walikuwa Athuman Machupa, Christopher Alex ambaye kwa sasa ni marehemu, Emmanuel Gabriel, Yusuph Macho ‘Musso’, pamoja na Ulimboka Mwakingwe ambapo katika mechi ya kwanza iliyopigwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Katika mchezo wa marudiano Simba ilifungwa bao 1-0 na kuzifanya timu hizo ziende kwenye penalti ambapo mlinda mlango, Juma Kaseja aliokoa moja huku Christpher Alex 'Massawe' akifunga penalti ya mwisho na kupeleka shangwe mitaa ya Msimbazi.


Yanga acha kabisa



 NA MSHAMU NGOJWIKE
 YANGA acha kabisa! Jeshi kamili la timu hiyo limewasili jana jijini Dar es Salaam likiwa limejidhatiti kisawasawa baada ya kuweka kambi ya wiki mbili jijini Mbeya likijiwinda na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.
 Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara, watacheza na Azam FC katika mchezo huo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa Jumamosi wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo unasubiriwa kwa hamu kutokana na ukweli kwamba kwa siku za hivi karibuni timu hizo zimekuwa na uhasimu wa jadi kama inavyokuwa kwa mechi ya Simba na Yanga. 
Yanga iliweka kambi ya wiki mbili Tukuyu mjini Mbeya ikijifua kikamilifu kuhakikisha inamalizia hasira zake zote kwa Wanalambalamba hao ambao waliwafunga katika mchezo wa robo fainali michuano ya Kagame.
Wakiwa Mbeya, Wanajangwani hao waliweza kutembeza kichapo cha hatari kwa timu za mkoa huo zilizojipendekeza kutaka kucheza nayo bila kujua wana hasira na Azam.
 Katika mechi hizo, Wanajangwani hao walianza kutembeza kichapo kwa Kimondo FC ya Mbozi inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza cha mabao 4-1 mchezo ukichezwa Uwanja wa CCM Vwawa.
 Baada ya hapo mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, waliwachapa maafande wa Prisons ya Mbeya kwa mabao 2-0, kabla ya kuhitimisha kambi yao kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mbeya City.
 Katika kambi hiyo ya Mbeya, Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm, alionekana kuwa mbogo baada ya kutoa dozi ya mazoezi ya kufa mtu kiasi cha kuonyesha kuwa wamepania kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam.
 Kitu ambacho kimeibua hisia za watu wengi ni kitendo cha wachezaji wa Yanga kuendelea na mazoezi ya kupasha misuli baada ya kocha kumaliza programu jambo linaloashiria hatari kwa timu yoyote pinzani watakayokutana nayo.
 Wakati Yanga ikijinasibu kufanya vizuri katika mchezo huo wa Ngao ya Jamii, kwa upande wao Azam wameibuka na kuchimba mkwara mzito wakidai kuwa wembe waliowanyolea Kagame wameuongezea makali.
 Azam ilijichimbia visiwani Zanzibar ambako iliendeleza wimbi la ushindi chini ya kocha wake Mwingereza, Stewart Hall, ambapo kikosi hicho kimeshinda michezo 12 tangu kocha huyo kukabidhiwa majukumu hayo.
 Wakiwa Zanzibar waliweza kushinda michezo yao yote mitatu ya kirafiki wakianza kutoa kipigo cha bao 1-0 dhidi ya KMKM.
 Mchezo uliofuata waliongeza dozi kwa kuwafunga Mafunzo mabao 3-0 kabla ya kuhitimisha kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya maafande wa JKU.
 Kwa ujumla katika mechi zote 12 chini ya Stewart tangu arejee Juni mwaka huu, Azam imefungwa mabao mawili tu katika mechi ya kwanza kabisa dhidi ya Friends Rangers Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
 Baada ya hapo, nyavu za Azam hazijaguswa tena kuanzia kwenye mechi za kirafiki hadi Kombe la Kagame pamoja na hizi tatu za kirafiki Zanzibar ambazo makipa wa Azam hawajaokota mpira nyavuni. 
 Kutokana na maandalizi ya timu zote mbili ni wazi mchezo huo utakuwa wa aina yake ukitarajiwa kuhudhuriwa na mashabiki wengi ili kujua nani mbabe kwa mwenzake.
 Kihistoria hiyo itakuwa mechi ya nane ya Ngao ya Jamii kuchezwa nchini na ya tatu kuzikutanisha timu hizo.
 Kwa mara ya kwanza timu hizo zilikutana mwaka juzi na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0, mfungaji akiwa ni Salum Telela, mwaka jana tena Yanga ikaibuka na ushindi wa mabao 3-0, ambapo mawili yalifungwa na straika Mbrazil, Geilson Santona 'Jaja' na moja la Simon Msuva.

Tuesday, August 4, 2015

Breaking News Juma Duni ajiunga Chadema

Mmoja wa viongozi wa juu wa Chama cha Wananchi (Caf) Juma Hadji Duni amejiunga na Chama cha Demokrasia na Manendeleo (Chadema) mchana huu na kwamba wakati huu anapigiwa kura ili kumuidhinisha kuwa Mgombea Mwenza wa Chedema  katika mkutano mkuu wa chama unaendelea hivi sasa ambapo Edward Lowasa naye anapigiwa kura na kuteuliwa mgombea Urais wa Jamhuri  wa Tanzania.