Wednesday, February 3, 2016

Martha Nelson anogewa na muziki wa injili



MWIMBAJI wa nyimbo za injili na mcheza filamu za Bongo, Martha Nelson, ni moja ya waimbaji wa muziki huo ambao wanafanya vizuri katika tasnia hiyo kwa sasa.
Martha mama wa watoto watatu, licha ya kufanya vizuri Afrika Mashariki kwenye muziki wa injili, lakini amekuwa akipata nafasi za kuitangaza nchi katika maeneo mengine nje ya Afrika ikiwemo Ulaya na Marekani.
Mwanamama huyu anasema kwamba, muziki wa injili umekuwa ni kimbilio na kielelezo cha kumfanya atambulike kuwa ni Mtanzania popote anapokuwa anakwenda, hasa kwa sababu kazi zake zote amekuwa akitumia lugha ya Kiswahili.
Martha anasema ili kufanikiwa kwenye muziki wa injili  lazima ufuate miiko inayoongoza muziki huo nayo ni ukweli pamoja na kumshirikisha Mungu. Lakini lingine kuhakikisha kazi inayofanyika ni bora ambayo inaweza kukubalika ndani na nje Tanzania.
“Kazi ya muziki wa injili ni ngumu lakini ukimtegemea Mungu ni jambo linalowezekana kufanikiwa. Lakini kubwa kuliko yote ni kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili ya nani.
“Kwa mfano katika kazi yangu mpya iitwayo ‘Yupo Mungu Asiyeshindwa’ niliweza kumshirikisha Mungu kwa kiwango kikubwa naamini ndiyo sababu ya kazi hiyo kufanya vizuri kwa wakati huu.
“Naelewa kuwa si jambo rahisi lakini niseme kwamba muziki huu bado unahitaji nguvu ya ziada kuhakikisha unakuwa na kupaa zaidi ya ilivyo sasa kwa sababu inawezekana kwani tunayemtumikia ni mkuu zaidi ya yeyote,” anasema Martha.
Mwimbaji huyo anasema katika kazi hiyo mpya ina jumla ya nyimbo nane ambapo kwa sasa imeshatoka ingawa sokoni itaingia katikati ya Februari. Baadhi ya nyimbo zilizozopo kwenye albamu hiyo ni pamoja na Usifiwe Jehova, Amenitoa Mbali, Acheni Niimbe na nyingine nyingi.
“Kazi hii natarajia itaingia sokoni katikati ya Februari ili mashabiki wangu waweze kuniunga mkono, ingawa kubwa kuliko yote ni kuhakikisha ujumbe wangu wa Neno la Mungu unawafikia watu wote.
Hii ni albamu ya pili kwa Martha ambapo ya kwanza aliitoa miaka mitano iliyopita iliyokwenda kwa jina la Unawaza Nini.
“Baada ya kutoa albamu yangu ya kwanza nilikaa zaidi ya miaka miwili nikiandaa kazi mpya, lakini baadaye nilikaa tena miaka hadi kuingia studio na kurekodi video. Kwa lugha rahisi ni kwamba, kazi hii nimeifanya kwa muda wa miaka mitano.
“Sababu kubwa zilizonifanya kuamua kuchukua muda mrefu katika kazi moja ni kutokana na kutafuta ubora, unapotaka kufanya kitu bora lazima ufanye kwa umakini lakini kitu chenye uhakika, mimi nilifanya hivyo kwa kuamini kwamba ninaweza kufanya kitu bora hasa ikizingatiwa kuwa hii ni kazi ya Mungu lazima iwe bora,” alisisitiza nyota huyo.
Mbali na kufanya vizuri kwenye muziki, lakini katika tasnia ya filamu amefanya kazi nyingi ikiwemo Poster Shadow, Haki, Tutafika pamoja na nyingine nyingi. Juu ya sekta hiyo, Martha ameishauri Serikali kuhakikisha kuwa inaisimamia sekta ya filamu vizuri pamoja na sanaa kwa ujumla ili kuzalisha ajira nyingi zaidi.
“Tunahitaji sanaa iwe ni kazi rasmi ambayo inaweza kusimamia maendeleo ya uchumi kikamilifu. Naamini kuwa kwa kutumia njia hii itasaidia katika mapambano dhidi ya umasikini,” amesisitiza mkali huyo wa injili. 

Martha Nelson katika picha mbalimbali.






Tuesday, December 29, 2015

Hiki ndicho akilichokisema Prof: Jay

Mbunge wa jimbo la Mikumi mkoani Morogoro, Joseph Haule amesema kuwa leo ametimiza miaka 40 lakini akiwa na furaha kubwa kwani ndiyo amekabidhiwa rasmi ofisi ya Mbunge jimbo la Mikumi.

Katika taarifa yake yenye mameno machache kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Facebook alisema kwamba:-

Asante sana Mungu leo nimetimiza miaka 40 tangu Nimezaliwa .... I dedicate this birthday kwa watu wangu wote wa MIKUMI na leo ndio tumeifungua rasmi ofisi ya MBUNGE ya MIKUMI baada ya kukabidhiwa Funguo na kuifanyia Usafi kwa pamoja tayari kwa kusikiliza changamoto za wana mikumi, Ushauri na maoni ya jinsi gani tunashirikiana pamoja na wana Mikumi kuweza kuleta mabadiliko na maendeleo ya MIKUMI YETU... EEE MWENYEZI MUNGU TUSAIDIE!!!.


Akifanya usafi ofisini kwake


 Akila kiapo kuwa mbunge wa Jimbo la Mikumi

 

 Akiwa anaingia Bungeni kwa mara ya kwanza


 Akiwa kwenye kikao cha madiwani

Akitekeleza shughuli za maendeleo kwenye usimamizi wa barabara jimbo la Mikumi

Monday, December 28, 2015

Yanga wamfukuza Niyonzima

Uongozi wa Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, umemfukuza rasmi kiungo wake wa kimataifa raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu.

Taarifa ya uongozi wa Yanga imesema kwamba wameamua kuchukua maamuzi hayo kutokana na mwenemdo wa nyota huyo katika utendaji wake wa kazi lakini pia kwa sababu alivunja kipengere kwenye mkataba wake na Yanga.

TAARIFA KAMILI HII HAPA:


 

Saturday, December 26, 2015

Waporaji wauawa Mbagala Kuu


VIJANA wa wawili katika eneo la Mbagala Mkuu wameuawa na wananchi wenye hasira badaa ya kupora beki la mwanamke mmoja mkazi wa Mbagala Kuu.
Tukio hilo lilitokea katika mtaa wa njia ya jeshini lafajiri ya leo ambapo baada ya kupora vijana hao waliokuwa watatu wakiwa na mapanga, bisibisi na vyembe walikimbia hadi mtaa wa makonde ambapo ndipo walipokamatwa na kisha kushambuliw ana wananchi wenye hasira wakiwa na silaha za jadi. 
katika tukio hilo mmoja ya vijana hao aliweza kukimbia na kufanikiwa kupona lakini mmoja alikimbilia kwenye moja ya choo kilichokuwa kwenye moja ya nyumba za mtaa huo ambapo wananchi hao walimfuata na kutoa kisha kupiga ambapo alimkata kata kisha kumuunganisha na mwenzake ambao waliwekwa kwenye eneo la wazi kisha kuchomwa moto.
Hata hivyo walikuonekana baadhi ya kina mama wakilia na wengine wakilaani tukio la kuuawa kwa vijana hao ambao hadi sasa bado hawajaweza kutambulika majina yao.
Katika siku za hivi karibuni eneo la Mbagala Kuu wameibuka vijana ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya uporaji na uharibifu wa mali.
Desemba 24 mwaka huu mwanamke mmoja alipora kisha kubakwa na vijana ambao hawakufahamika mara moja wakati mwanamke huyo akitokea kazini majira ya saa 3:00 usiku.
Mbali na tukio hilo kumekuwepo na matukio ya kuvamiwa na kuporwa mali watu mbalimbali wakiwa kwenye mageti ya nyumba zao wakiwa wanasubiri kufunguliwa jambo lililozusha hasira kutoka kwa wananchi mbalimbali wa kato hiyo.

Thursday, December 24, 2015

Yanga yapeleka majina 24 CAF




NA SAADA SALIM
KOCHA Mkuu wa Yanga Mholanzi, Hans Pluijm, ana hasira za msimu uliopita kushindwa kuifikisha timu hiyo pazuri kwenye michuano ya kimataifa lakini safari hii ameapa lazima kieleweke.
Unajua kwanini? Mholanzi huyo safari hii amepeleka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), majina ya silaha zake 24 huku 10 zikiwa za kimataifa tayari kwa kufanya makubwa mapema Februari mwakani kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika majina hayo 24 ukiwaacha, Thaban Kamusoko, Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima, Issoufou Boubacar Garba, Vicent Bossou na Mbuyu Twite, Pluijm ameamua kuleta majembe mengine mawili ya kimataifa ingawa tayari inaye mchezaji mmoja Mnyarwanda, Jerome Sina, anayefanyiwa majaribio.
DIMBA Jumatano limethibitishiwa kwamba Yanga itawaleta straika, Spencer Sautu kutoka Ashanti Gold ya Ghana, ambaye ataungana na beki shupavu aitwae Kabongo kutoka Congo (DRC).
Wawili hao wanakuja wakati wowote nchini kuanzia sasa kufanya majaribio ingawa inaelezwa kwamba kocha Hans anavifahamu vyema viwango vyao vya soka.
Chanzo cha habari cha uhakika kimelieleza gazeti hili kuwa ujio wa wawili hao utafanya timu hiyo iwe na wachezaji 10 wa kimataifa ili kukifanya kikosi chao kiweze kuhimili vishindo vya michuano hiyo mikubwa zaidi barani Afrika na yenye utajiri mkubwa inayoandaliwa na CAF.
Aidha, chanzo hicho kilieleza kuwa Yanga bado inaendelea kumfanyia majaribio kiungo wa Rayon Sport, Jerome Sina, ingawa usajili wake utasubiri kwanza ili kulinganishwa kiwango na Sautu.
Jerome mwenye miaka 26 raia wa Congo (DRC) amemvutia Pluijm na inaelezwa iwapo atafuzu majaribio atasajiliwa mwishoni mwa msimu kwa ajili ya kuibeba Yanga.
"Sasa hivi hatutaki masihara kwani tunahitaji kufika mbali zaidi, ukiangalia msimu uliopita hatukufikia malengo yetu kwa vile tulitolewa mapema ndiyo maana usajili wa wachezaji wa kigeni unafanyika kwa umakini mkubwa tukiamini watasaidiana vyema na wazawa ili mwakani tuweze kuvunja rekodi yetu," alisema mtoa habari.
Alisema tayari benchi la ufundi la timu hiyo limependekeza kupeleka idadi ya majina 24 kwa ajili ya michuano hiyo ya kimataifa ambapo wachezaji hao wawili wanaotarajia kutua hapa nchini wataungana na Sina kwa ajili ya majaribio na baadaye kusaini.
Katika hatua nyingine, Yanga imebadilisha mipango yake ya kwenda kujifua nchini Ghana kwa ajili ya kujiandaa na michuano hiyo na badala yake watabaki hapa nchini na kuzialika timu za nje ili kucheza nazo mechi za kujipima.
Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm, ameliambia DIMBA Jumatano kuwa wana mpango wa kuzialika timu tatu za kimataifa ambazo ni Ashanti Gold ya Ghana pamoja na Gor Mahia na KCB zote za Kenya.
"Mpango wetu wa kwenda nje ya nchi umekufa kutokana na ratiba kuingiliana, lakini tumezialika timu nne ambapo mbili za KCB na Gor Mahia tayari zimethibitisha huku Ashanti ikiwa bado," alisema kocha huyo.

Tuesday, October 27, 2015

Busungu, Maguli waitwa Stars

Busungu 
 
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Charles Boniface Mkwasa, jana alitangaza kikosi cha timu hiyo kitakachovaana na Algeria, huku akiwaita mastraika wanaotisha kwa kutupia nyavuni, Malimi Busungu wa Yanga na Elius Maguli wa Stand United waje kukinogesha.
Stars na Algeria zinatarajia kuvaana Novemba 14 jijini Dar es Salaam katika mechi ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kufanyika jijini Moscow, Russia, mwaka 2008.
Timu hiyo imefanikiwa kuvaana na Algeria katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kupangwa kwenye makundi baada ya kuitoa Malawi katika hatua ya kwanza.
Mkwasa amemuongeza Maguli ambaye amekuwa katika kiwango bora kwenye msimamo wa wafungaji bora wa Ligi Kuu Bara, akiwa na mabao nane wakati Busungu yeye akiwa na mchango mkubwa katika kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga, ambapo pia amefunga mabao mawili kwenye msimamo wa wafungaji wa ligi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, Mkwasa ametaja wachezaji 28 ambao watakwenda kambini Oman Novemba 2, mwaka huu.
Mkwasa amewataja wachezaji wengine walioitwa kuwa ni makipa, Aishi Manula (Azam FC), Ally Mustafa 'Barthez' (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
Mabeki ni Shomary Kapombe (Azam FC), Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan (Yanga SC), Hassan Ramadhan Kessy, Mohammed Hussein 'Tshabalala,' Hassan Isihaka (Simba SC) na Salim Mbonde (Mtibwa Sugar).
Viungo ni Himid Mao, Mudathir Yahya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo (Azam FC), Jonas Mkude, Said Ndemla (Simba SC) na Salum Telela (Yanga SC), wakati washambuliaji ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Free State Stars, Afrika Kusini), Farid Mussa, John Bocco (Azam FC), Simon Msuva, Malimi Busungu (Yanga SC), Elias Maguli (Stand United) na Ibrahim Hajib (Simba SC).
"Kikosi hicho kitaingia kambini Novemba 1 katika hoteli ya Urban Rose, Dar es Salaam, kabla ya safari ya Muscat, Oman kwa kambi ya siku 10.
"Tukiwa Oman, pamoja na mazoezi, tutacheza mchezo mmoja au miwili ya kujipima na wenyeji wetu, iwapo watakuwa tayari kabla ya kurejea Dar es Salaam Novemba 11 tayari kwa mchezo wa kwanza na Algeria Novemba 14, Uwanja wa Taifa,” alisema Mkwasa.
Alisema kikosi hicho kitaondoka Dar es Salaam kwenda Algiers Novemba 16 mwaka huu, tayari kwa mchezo wa marudiano Novemba 17, nchini Algeria.

Wednesday, October 14, 2015

Habari njema kwa watu wote

KAMPUNI YA WAZALENDO BRIGHT MEDIA Inatoa punguzo kwenye huduma zake kuanzia Septemba Mosi 2015 hadi Januari 30, 2016. Tuduma zinazotolewa ni pamojana Kuandaa mikutano na Waandishi wa habari, kuandaa matangazo ya redio, tv na magazeti, Logo aina zote, Mabango makubwa na madogo, Diary, Business Cards, Video Productions, Vehicles Branding, Vipindi vyote vya Tv na Radio ikiwemo filamu.
Pia tunatengeneza websites na blogs.
Njoo upate bidhaa bora kwenye kampuni bora. Tupo Ilala, Kinondoni na Temeke.
Wasiliana nasi kwa namba.
+255 784 890 387
Email: nellymtanzania@gmail.com
Pia tunapatikana kwenye www.dirayaulimwengu.blogspot.com
Hizi ni baadhi ya bidhaa zetu.

  
Zifuatazoni miongoni mwa kazi zilizofanywa hivi karibuni.